Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
umeeleza vizuri sana, Philip morris au kwa kifupi "PMI" ndio mnunuzi mkubwa wa tumbaku inayozalishwa Tanzania chini ya Alliance one na Tltc(30mil kg, kwa makadirio),Ninachojua mimi kiwanda kile wanachokiita MOIL ni cha PMI_Philip Moris Inc(Wamarekani)
Kilianza kufanyakazi mwaka wa jana kama mtakumbuka vizuri mbio za mwenge kiliweka jiwe la msingi na pia Prime Minister alishakitembelea na sigara zao nafikiri zimeingia sokoni (Marlborro)
Pale nilichojua mimi MOIL kama mtanzania ambaye ndio mbia wa kitanzania ndio anawafanyakazi hao 200.
kile kiwanda kimefungwa mitambo ya kisasa sana inaowezesha kuendeshwa na wafanyakazi wachache saaana kama tujuavyo zao la Tumbaku ni la msimu kwahiyo kitakuwa na wafanyakazi wachache waajiriwa na watakaobaki wa msimu kama wenzao wa Alliance One ambao wanawaajiri wachache wasiozidi 400,
waliobaki zaidi ya 2100 wa msimu kutokana na zao lenyewe.
Najua kwa sasa kiwanda kina wafanyakazi wasiofika 90 lakini wanalipwa vizuri saana kutokana na wateja walengwa
na wamelenga soka la Africa kwa ujumla.
Waajiriwa wengi ni watanzania ,wizara ya mambo ya ndani kwa sasa ipo makini saana na work permit kulinda soko la ajira kwa wazalendo
Wadau wanaojua zaidi watakuja kufafanua zaidi.
alliance one na tltc wana viwanda vikubwa sana hapo morogoro lakini hawatengenezi final product Bali wanafanya processing then inasafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kutengenezwa final product, sasa kitendo cha wao kuja kufungua kiwanda ambacho kinatengeneza final product hapahapa nchini ni jambo kubwa sana na la kimaslahi kwa taifa.
kwa kuweka kumbukumbu sawa kiwanda cha sigara cha TCC kinamilikiwa na JTI na JTi sio mnunuzi mkubwa sana wa tumbaku Tanzania ukilinganisha na Philip morris, hvyo hicho kiwanda kitakuwa kikubwa sana chenye tija!
[HASHTAG]#uvutaji[/HASHTAG] wa sigara ni hatari kwa afya yako#