Kiwanja cha futi 40 kwa 50 kinatosha kujenga nyumba?

Edward wa kwetu

New Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Wataalam naomba mchango wenu wa mawazo.

Hivi kiwanja chenye ukubwa wa futi 40 kwa futi 50 kinaweza kutosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu sebule public toilet na jiko.

Naomba mwenye uzoefu anisaidie hili
 
Hicho n sawa na meter 12 kwa 15 ambapo n sawa na 180 square meter, kinaweza kutosha kama utajenga nyumba yenye vyumba vya ukubwa wa kawaida tu sio vile vikubwa sana ila tu hutopata sehem hata ya parking ya gari kwa ukubwa huo, na unatakiwa upangilie vizur position ya kuiweka nyumba ili upate sehem hata ya kuchimba shimo la choo.

NB:: usipende kununua kiwanja kikiwa kimepimwa kwa vipimo vya futi kama huna ujuzi mzuri wa kudeal na namba za vipimo, kipimo cha futi kinawachanganya sana wengi unaweza kuona kama umepata kiwanja kikubwa sana kumbe n cha kawaida tu.
 
Maelezo haya yanajitosheleza
 
Wataalam naomba mchango wenu wa mawazo.

Hivi kiwanja chenye ukubwa wa futi 40 kwa futi 50 kinaweza kutosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu sebule public toilet na jiko.

Naomba mwenye uzoefu anisaidie hili
Utajenga lakini hata pakuchimba choo hupati
 
Umemaliza kula kitu
 
Wataalam naomba mchango wenu wa mawazo.

Hivi kiwanja chenye ukubwa wa futi 40 kwa futi 50 kinaweza kutosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu sebule public toilet na jiko.

Naomba mwenye uzoefu anisaidie hili
Mkuu kama alivyoreply RWANTANG, hapo unatoa nyumba nzuri ya wastani yenye kila kitu, parking gari yako na wife, banda la kuku na kasehemu kakuchezea watoto. Ndio itakua imejibana lkn sio kiivyo. Naishi kwny nyumba kiwanja mita 9x14 sawa na futi 30 kwa 47 Ina izo facilities zote nilizozitaja except ina vyumba 2. Karibu
 
Wataalam naomba mchango wenu wa mawazo.

Hivi kiwanja chenye ukubwa wa futi 40 kwa futi 50 kinaweza kutosha kujenga nyumba ya vyumba vitatu sebule public toilet na jiko.

Naomba mwenye uzoefu anisaidie hili
Bila shaka kiwanja kipo chamazi au vikindu mana ndo wanapima kwa futi. Ovyo kabisa!
 
Siku ukifa tutaagia kanisani hakuna hata sehemu ya kuweka jeneza lako wala kufunga turubai la msiba
 
Unajenga lakini iwe nyumba ya ghorofa.

Sebule utaweka sakafu ya chini pamoja na jiko, ghorofa la kwanza utaweka room 1 ya kulala na stoo, ghorofa ya 2 utaweka chumba cha kulala kikiwa na choo na bafu.

Ukitaka kuongeza vyumba utaongea kwa njia ya ghorofa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…