Kiwanja nilichonunua Tsh. Milioni 4 kilivyonipa zaidi ya Tsh. Milioni 20

Ardhi haina uongo. Mimi mara yangu ya kwanza nilinunua sehemu kwa mda ule ni shamba lakini kwa sasa ni viwanja na nilipata kwa sh laki 8 tu kuandkisha wakala 20 mashahidi kreti la bia mda huo bia inatoka sh800 had sh900. Viwanja nilivikata nikapata zaidi ya viwanja kumi vya kujenga nyumba tena kubwa. Sasa hivi sio siri bila kuanzia mil12 huwezi kupata kiwanja pale na hata usinipgie cmu ati unataka kiwanja kwangu na kila mwaka panaongeza dau. Kuna mwana jf alikuja na uzi akiambia watu kuwa ukiwa na pesa nunua viwanja kwa wingi watu wakambeza kweli. Lakin ukweli ardhi haidanganyi. Usikimbilie mijini coz viwanja vya mijini vingi vina migogoro nunua huko mashamban mwisho wa cku utakuja kula vizuri. Nani angelijua sehemu kama kerege huko bagamoyo pangelikuwa na soko na ni sehem ambayo kila mtu alikuwa anaona kuwa wanaoish huko hawana akili lakin sasa hivi%¿?\/
 
Nilivuoona huu uzi nimeikimbilia sana Kuna eneo nimeambiwa million 4 ila pembeni kidogo inabidi nilifuate tu
 
Dah wewe ni hasara sana.
Yaani kama wewe ndio mtoto wangu halafu nagundua una mawazo hayo nakuwahi nauza kabisa naenda kuishi hotelini au kwenye apartment za kupanga ili tuone utauza nini
 
Nilivuoona huu uzi nimeikimbilia sana Kuna eneo nimeambiwa million 4 ila pembeni kidogo inabidi nilifuate tu
wahi mkuu usisikilize maneno ya wakatisha tamaa.
Mimi kuna mahali nilinunua kiwanja kwa milioni 4 miaka 13 nyuma.
Sasa hivi kuna wachaga fulani walivikusanya vingi sasa hivi wanauza kwa milioni 40.
Yaani hadi najilaumu kwa nini sikununua viwanja vingi angalau vitano
 
😂😂😂Akili ya mitoto mivivu!baba yangu ana eneo lake flani limepanda sana bei huwa namtania mzee uza utugawie kamtaji kiasi kiasi watoto wako wote,zinazobaki kula malizia uzee wako maana ukifa,tukimaliza 40 tu hili eneo tunauza...mzee kakaza,nadhani ana lengo jema na watoto wake😂
 
Sophy umenikumbusha mbali sana
2022 kuna jamaa alihitaji laki 4 kwangu. Nilimpa. Baada ya miezi mitatu akaniambia ameshindwa kulipa, nimuongezee laki 3 anipe kiwanja. Kiwanja kilikua kidogo, na kipo mahali hapajachangamka so sikukipenda. Ila kwakua ni jamaa angu nilikubali.

2023 nilihitaji kiasi flan, nikakiuza mil 2.2. Hapa eneo lilishaanza kuchangamka, na neighborhood yake imestaarabika na ina hadhi.

2025 aliyekinunua kwangu akapata uhitaji wa ghafla, na hakufanya transfer so mtu wakwanza kumtangazia nikawa mimi. Ila alikomaa mil 5. Nikakomaa nikachukua kwa 3.5

Mimi sasa mwaka huu nimekiuza mil 9, kwa mwanasheria kalipa mteja, mimi hela yangu nimepokea kama ilivyo.. Kiwanja kina neighborhood yenye hadhi sana, ila tu chenyewe ni kidogo.
Nikasema kumbe watu wa real estate ndo wanafaidi hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…