Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wakati maelfu ya wapalestina wakiuliwa kama kuku,viongozi wa nchi za kiarabu walipiga kimya na kula biriani zao wakiona hayo hayawahusu.
Hata diplomasia zao na kulaani kulikuwa kwa njia za kinafiki.
Baada ya kumfanya Netanyahu ajiamini kupiga apendapo na kuamua kuipiga Iran na Iran nayo kutofanya ajizi kwa kujibu pigo hilo kwa ujasiri mkubwa. Sasa viongozi wa nchi za kiarabu ndio wameanza kuamka na kuanza kupigiana simu wakiulizana nini kimetokea na nini wafanye.
Kiwewe hicho kimeongezeka sana tangu juzi baada ya kudhihirika Israel imekusudia kuficha aibu kwa kuamua kuipiga Iran huku na Iran nayo ikipandisha mori na kusema ikiguswa tena itajibu kwa nguvu kubwa na kwa kutumia silaha kali zaidi na kuahidi kuanza na vinu vya nyuklia vya Israel.
Simu zimekuwa hazsikae tena mezani kati ya wafalme wa UAE na Saudi Arabia.Kwa upande mwengine Qattar nayo imechanganyikiwa kwani ina askari 10,000 wa Marekani na kambi kubwa ya kijeshi ya nchi hiyo.
Katika mazungumzo yao hayo viongozi hao wamekuwa wakiijadili Jordan na hatari inayoinyemelea ya kuzidiwa na wimbi la vuguvugu kutoka Iran litakalotoa lango la Iran kuifikia Quds.