Kiwewe kizito chawakumba walioshiriki au kushirikishwa katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu!

Kiwewe kizito chawakumba walioshiriki au kushirikishwa katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu!

Ilikuwa ni swala la muda tu...malipo ni hapa hapa duniani! Adolf Hitler alikuwa na Heinrich Himmler, Idi Amin alikuwa na Isaac Maliyamungu na sisi tunaye A.D.Bashite.
 
Muda ndio huu,ukweli kujulikana.
"******* we washughulikie ndani,mi nitawashughulikia nje" By........
 
Ilikuwa ni swala la muda tu...malipo ni hapa hapa duniani! Adolf Hitler alikuwa na Heinrich Himmler, Idi Amin alikuwa na Isaac Maliyamungu na sisi tunaye A.D.Bashite.
Abacha alikuwa na Mustapha bashite mdogo aliyeogopwa hadi na majenerali Wa Nigeria heri uitwe na abacha na mustapha majenerari wazima wanaenda wakitetemeka ,kila jambo linamwisho mustapha aliuliwa kwa sumu,maliyamungu alikufa ajulikani.
Dunia aijawahikoma funza wasiofunzwa.Mwisho umefika
 
Machadema bana yanapenda kujifurahisha kweli. Hicho unachokiita kiwewe kizito kipo wapi? Unafikiri hili tukio la Kibaraka Lissu litabadili fikra za wazalendo kwenye utawala huu? Hakuna kitachobadilika na kwa kuwa hamuhitaji msaada kutoka upande wa pili basi muendelee kumuuguza mgonjwa wenu na sisi tutaendelea kulitumikia taifa kama kawaida haturudi nyuma na vibaraka wote lazima wanyooshwe!
shetani huja kwa njia nyingi sana.
 
Mzee Mkaqpa mpka leo anatubu kuhusu mauaji ya wapemba, dhamira yake ina msuta mpaka leo, watawala mjifunze kwa hilo kuna kesho ya duniani na mbinguni.
 
Kuna viti watu wamevikalia ambavyo vinaanza kupata joto na waliovikalia lazima kiwewe kizito kiwakumbe...ngoja tuisubiri hiyo Oktoba 28!
 
DUA zetu zitajibu tu.
hata kama sio kesho basi kesho kutwa!
Dua zimeshajibu na hivi sasa kiwewe chazidi kushika kasi huku joto la viti walivyovikalia likizdi kupanda na muda si mrefu wataanza kuumbuana asubuhi asubuhi wakitajana kwa majina.

Wote walioshiriki katika jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu wanazidi kuteseka baada ya kiongozi wao mkuu kusalimu amri kwa korona...malipo ni hapa hapa duniani.
 
Wewe humu jf kutwa unadhihaki watu Dua gani utatuma liwapate waliopewa nguvu na Mungu kuongoza Taifa? Mnafikiri kuongoza nchi ni sawa na Kuongoza Familia... Ajari ya Lissu anaweza pata yeyote ila kuombea Dua baya kwa waliotenda ni mbaya kwako even Yesu aliwasamehe hadi waliomchoma mkuki mbavuni... akiwaambia hawajui walitendalo japo walikuwa wamedhamilia... Kuombea watu Mabaya wadhania Dua hiyo itapokelewa as if wewe ni msafi sana.. Wewe Muombee tu Lissu apone kabisa na uombee na wengine Duniani walio kwenye Majanga hata zaidi ya Lissu Wapone kisha tubu dhambi zako.
Ohoo, wewe endelea na ndoto zako huku watu wakizidi kupukutika wa kwanza akiwa yule dhalimu mkuu aliyesalimu amri kwa corona!
 
Je safari hii pandora box litafunguliwa? Je tunao ujasiri wa kuchungulia ndani ya hilo pandora box? Naona tunaanza kupata fununu japo kwa mbali kuhusu wale waliodaiwa kutojulikana...wale watekaji, watesaji na watupaji (wa miili)... RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda na RIP Watanzania kibao ambao hadi leo hii haijulikani walipotelea wapi!

Je kiwewe kilichowakumba waliopanga na waliotekeleza jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu A. Lissu hatimaye kitafungua mlango wa hilo box? Je giza zito lililotanda na kuwafunika wasiojulikana taratibu linaanza kutoweka na mwanga mdogo kupenyeza? Je kesi feki ya Mbowe itawazindua Watanzania wautambue ugaidi kwa sura yake halisi?

Tuvute subira ndugu zangu kwani machozi ya wote waliopotelewa na ndugu zao pasi shaka hayatapotea bure!
 
Na bado mtafarijiana sana lakini mwanzo wa mwisho wa walio panga kumuua Lissu umeshaonekana! Mara paap kiongozi wa wasio julikana kafa! Tutakula na kunywa mpaka asubuhi bill anatulipia Mungu.
Mara paap na kweli ikawa hivyo…hii dunia ina maajabu yake!
 
Back
Top Bottom