Kiza Hussein Mayeye: Nikishukuru sana chama changu cha CUF kwa kuniamini na kunipa nafasi

Kiza Hussein Mayeye: Nikishukuru sana chama changu cha CUF kwa kuniamini na kunipa nafasi

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
IMG_20200619_111153_561.jpg
Kwanza kabisa nianze Kumshukuru mwenyezi mungu kwa afya njema na kunisimamia katika kipindi changu chote nikiwa kama mbunge.

mimi kwa majina naitwa Kiza Hussein Mayeye ,nimzaliwa wa Kigoma katika kijiji cha mwandiga.elimu yangu ya msingi niliipata katika shule ya msingi mwandiga ambapo nilimaliza darasa la 7 mwaka 2000.

2015 niligombea ubunge kwa kujaza form ya jimbo la kigoma kaskazini lakini na viti maalumu,kupitia chama cha CUF, lakini sikusimama jimbo kwani tulikua na ukawa na kuwaachia Chadema na nilibaki viti maalumu,
baada ya mgogo wa CUF niliichaguliwa kuwa mbunge mwezi wa 7/2017 na niliapishwa rasmi tar 5/9/2017 hivyo nimetumikia ubunge wangu kwa miaka 3.

kwa upande wa changamoto katika kipindi changu cha ubunge zipo nindogondogo za kibinadamu ambazo wala siyo kubwa kusema nisizisahau ama ziliniumiza sana hapana ,nashukuru Mungu kwa miaka 3 nimefanya kazi zangu vizuri sana ushirikiano ndani ya chama ,watanzania,wanakigoma ,na wabunge wenzangu wote bungeni bila kujali vyama vyao nimeishi nao vizuri sana na kujifunza mengi sana ,nawashukuru sana.

kwa upande wachangamoto ambazo nimewahi tatua mkoani kigoma ,kwanza ni kero ya maji kiukweli mbali na kuwa na ziwa tanganyika ,mto maragalasi lakini bado vijiji vingi vinashida ya maji,sasa ilipoingia bungeni kero ya maji nijambo ambalo nililiwakilisha vizuri sana katika kuhakikisha naieleza serikali juu ya namna kina mama wanavyohangaika umbali mrefu kutafuta maji safi na salama kwa kujata vijiji ambavyo wanainchi wanateseka sana ikiwepo kijiji nachozaliwa mwandiga ambapo nami nimebeba sana maji kutoka mungonya,nkema ,hivyo nilieleza kwamba sasa tumechoka tunataka maji ,na ninashukuru sana hilo walilisikia serikali na sasa katika kijiji cha mwandiga maji kero imepungua na mradi unaendelea ili tuweze kupata maji ya uhakika 24/7 na maeneo mengine pia yatafikishiwa mradi wa maji wa ziwa tanganyika ,hii ni hatua kubwa sana nayojivunia kwa kuwawakilisha vyema wanainchi wangu wa kigoma.

lakini suala la uhuduma za afya ,nimekua mstari wa mbele katika kutetea huduma bora ya afya katika mkoa wangu wa kigoma na tanzania kwa ujumla,kwani kila niliposimama hasa katika budget niliieleza serikali namna watanzania wanavyoteseka katika maeneo mengi kupata huduma za afya kwani kina mama wanatembea umbali mrefu kutafuta hosp ,hali hiyo kupelekea vifo vya mama na mtoto ambapo kwa mkoa wangu kigoma nivingi,hivyo nimekua nikiomba serikali iongeze vituo vya afya katika vijiji vyetu lakini wauguzi wa kutosha kwani bado tunauhaba wa wauguzi katika hospital zetu.

lakini nakumbuka katika bunge la budget ya 2018/2019 nilipigia kelele suala la wataalamu(specialist)katika hosp yetu ya mkoa wa kigoma maweni,na vifaa kama citi scan,xray mashine kwamba nichangamoto kubwa katika hosp yetu ya mkoa ,serikali ilipokea na tulipata wauguzi katika hosp zetu walioongezwa na kuahidi kutatua kero hizo za vifaa ,haya kwangu nimafanikio kwa wanakigoma ingawa bado changamoto zipo Mungu anisaidie nirudi bungeni ili niendelee kuileza serikali, kuishauri na kuilekeza juu masuala ya afya katika mkoa wa kigoma na tanzania kwa ujumla.

lakini pia natambua bado sekta ya afya hata wauguzi wanachangamoto hasa katika suala la mshahara mdogo, makazi duni ,nalo nimekua nikilisemea sana ili serikali ione namna gani inaboresha miundombinu hiyo lakini na kuwakumbuka katika nyongeza ya mishahara na haki zao zote hali kadhalika kwa walimu wetu.

lakini kwa kutambua umuhimu wa afya na kujali wanainchi wa kigoma nimekua mdau wa kuchangia mambo mbali mbali katika ujenzi wa hosp ambao wanainchi wanajitolea kujenga kama bubango ambapo niliweza changia mifuko ya cement,
pia mafanikio mengine ya ubunge wangu kigoma nimengi kwani nimekua mdau wa masuala ya kuchangia jitihada zinazofanywa na wanainchi kwa kuchangia mambo mbali mbali katika ujenzi wa shule,lakini katika kushirikiana na vikundi vya kinamama na vijana katika kuona namna gani mimi kama kiongozi tunasaidiana ,kushauriana katika kuondokana na dimbwi la umasikini na ukosefu wa ajira,hivyo nimekuwa niki support baadhi ya vikundi,watu katika kuona namna gani tunapambana na ugumu wa maisha .

Tukirudi katika chama changu cha CUF kwakweli kwanza nikishukuru sana sana kwa kuniamini na kunipa nafasi kubwa kwanza nikiwa na umri mdogo lakini waliamini brain yangu kuliko kujali umri nashukuru sana, hasa Mwenyekiti wangu Taifa Prof Ibrahim Haruna Lipumba,hakika sina cha kuwalipa chama changua isipokuwa nawaahidi kukitumikia kwa hali na mali kwa uaminifu mkubwa sana.
Kwa upande wa nimefanya nini katika chama kwakweli nimengi sana na makubwa na kwa wana CUF nimashahidi nimetumia muda ,rasilimali zangu katika kuhakikisha naijenga CUF kigoma ambapo kama Mbunge wa CUF leo najivunia na ninaweza kusema kwa muda mchache nilisimama na wanainchi wakigoma bila kujali itikadi ya mtu na kusimama imara na kutetea maslahi yao.
lakini nimeshirikiana vyema na jamii kama Mbunge wa CUF bila kujali itikadi kwa kuzingatia misingi ya chama changu ya HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE

lakini naweza kusema nawakilisha mkoa mzima wa kigoma nimejitahidi kufika na kufanya kazi ,lakini kuwa karibu na viongozi wote wa mkoa mzima kuhakikisha tunaijenga CUF bila kuchoka kwa hali,mali ,na ushauri mbali mbali na ninaweza kusema kigoma CUF tunauongozi imara na unaojitambua katika kutekeleza majukumu yao,hii najivunia kwani nikutokana na mimi kuwaamini viongozi wangu lakini kuelekezana nao nini tufanye haya nimafanikio kwetu kama chama na uongozi.

lakini mbali na kuwakilisha mkoa mzima wa kigoma ,sikusita kuzunguka maeneo mengine ya tanzania kuijenga CUF yangu kwa garama zangu, naweza sema nimmoja ya wabunge ambao nimefika maeneo mengi kuijenga CUF kwa garama zangu lakini na kutimiza ahadi mbalimbali kwa wanainchi.
nimefanya kazi ya ujenzi wa chama katika maeneo mengi aidha kwa kufika ama ku support jambo la ujenzi wa chama kama

1.Dar es salaam
2.Tanga
3.Arusha
4.morogoro
5.Dodoma
6.Mwanza
7.Tabora
8.Kusini
9.Mbeya
10.Bukoba hayo kwa uchache,lakini nilifanya bila kujali kwa kuamini CUF nimoja.kiukweli nimengi sana ambayo nimefanya ndani ya CUF siwezi yamaliza yote lakini kubwa naipenda CUF na nipo tayari kuitumikia kwa hali na mali bila kuchoka.

Mwisho niseme tunakwenda katika uchaguzi mkuu October kwanza niombe sana serikali uchaguzi uwe wa huru na haki,na ninashukuru Rais wetu ameshatuhakikishia hilo
Hivyo niwaombe watu wengi kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali katika maeneo yetu hasa kina mama ,tuamini tunaweza tusimame katika majimbo kuanzia ubunge ,udiwani hata Urais pia katika vyama vyetu ,tujiamini tusiyumbe kwa namna yeyote ile mama ni shujaa siku zote.

lakini vijana pia tusibaki nyuma tuamini tunaweza kufanya makubwa tuwatumikie wanainchi wetu kwa moyo wote kwani ubunge ni wito ingawa wapo wengine hawadhani kama niwito kwani maslahi mbele kuliko kero za wanainchi.

Na mwisho niseme mimi nimeamua kuomba ridhaa kwa wanakigoma kaskazini october kusimama jimbo la kigoma kaskazini ili nipate ridhaa ya kurudi bungeni kama mbunge wa jimbo nikaendeleze yale ambayo tayari nimeanza kuyafanya katika kipindi changu cha miaka 3 ya ubunge wangu ,sina shaka na wanakaskazini kwani wanajua jitihada zangu kwa muda mfupi juu yao.

Namshukuru Mungu kwa yote kwangu,nawashukuruni sana wana CUF kwa kuniamini,nawashukuru sana wanakigoma na watanzania wote kwakua pamoja nami katika kipindi hiki cha miaka 3 ya ubunge wangu. sina cha kuwalipa nawaomba tusimame imara katika kusimamia Rasilimali za inchi yetu, tusimame imara katika kuilinda amani na utulivu wa inchi yetu tuliyonayo,tupendane,tushirikiane,tuheshimiane na tuenzi yote mema yaliyofanywa na viongozi wetu ,Bibi,Babu na wazazi wetu. Inshaallah kila mwenye kuamini yupo pamoja na Mungu. nawapenda wote
Asanteni.
 
Waweza kupewa kwa amri ya mkulu,lakini mazingira yanaonesha kama kikundi chenu baada ya kutumika na dola sasa mmeshachuja wamesajiliwa NCCR nw
 
IMG_20200619_120205_917.jpg
T

Ukirudi katika chama changu cha CUF kwakweli kwanza nikishukuru sana sana kwa kuniamini na kunipa nafasi kubwa kwanza nikiwa na umri mdogo lakini waliamini brain yangu kuliko kujali umri nashukuru sana, hasa Mwenyekiti wangu Taifa Prof Ibrahim Haruna Lipumba,hakika sina cha kuwalipa chama changua isipokuwa nawaahidi kukitumikia kwa hali na mali kwa uaminifu mkubwa sana.

Kwa upande wa nimefanya nini katika chama kwakweli nimengi sana na makubwa na kwa wana CUF nimashahidi nimetumia muda ,rasilimali zangu katika kuhakikisha naijenga CUF kigoma ambapo kama Mbunge wa CUF leo najivunia na ninaweza kusema kwa muda mchache nilisimama na wanainchi wakigoma bila kujali itikadi ya mtu na kusimama imara na kutetea maslahi yao.

lakini nimeshirikiana vyema na jamii kama Mbunge wa CUF bila kujali itikadi kwa kuzingatia misingi ya chama changu ya HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE

lakini naweza kusema nawakilisha mkoa mzima wa kigoma nimejitahidi kufika na kufanya kazi ,lakini kuwa karibu na viongozi wote wa mkoa mzima kuhakikisha tunaijenga CUF bila kuchoka kwa hali,mali ,na ushauri mbali mbali na ninaweza kusema kigoma CUF tunauongozi imara na unaojitambua katika kutekeleza majukumu yao,hii najivunia kwani nikutokana na mimi kuwaamini viongozi wangu lakini kuelekezana nao nini tufanye haya nimafanikio kwetu kama chama na uongozi.

Lakini mbali na kuwakilisha mkoa mzima wa kigoma ,sikusita kuzunguka maeneo mengine ya tanzania kuijenga CUF yangu kwa garama zangu, naweza sema nimmoja ya wabunge ambao nimefika maeneo mengi kuijenga CUF kwa garama zangu lakini na kutimiza ahadi mbalimbali kwa wanainchi.

Nimefanya kazi ya ujenzi wa chama katika maeneo mengi aidha kwa kufika ama ku support jambo la ujenzi wa chama kama

1.Dar es salaam
2.Tanga
3.Arusha
4.morogoro
5.Dodoma
6.Mwanza
7.Tabora
8.Kusini
9.Mbeya
10.Bukoba

Hayo kwa uchache,lakini nilifanya bila kujali kwa kuamini CUF nimoja. Kiukweli nimengi sana ambayo nimefanya ndani ya CUF siwezi yamaliza yote lakini kubwa naipenda CUF na nipo tayari kuitumikia kwa hali na mali bila kuchoka.
 
Back
Top Bottom