ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Sisi wa kizazi chetu before gen Z tulienjoy maisha kwa vitu ambavyo watoto wa leo wanaweza wasivielewe. Tulikula zambarau na maapera ya mtini, tukachezea magari ya plastiki, na sikukuu tuliisubiri kwa hamu kana kwamba tunasubiri matokeo ya mtihani. Siku ya sikukuu ukipata nguo mpya, hata kutumwa dukani ulikuwa unaenda kifua mbele.
Wali ukipikwa, kazi yetu ilikuwa kupita jikoni kila baada ya dakika tano kuuliza: “Mama, tayari?” Ukiambiwa bado, unarudi tena
Tuliruka kamba, tulicheza kombolela na kujificha, tukasukuma tairi barabarani, na wakati mwingine mchezo mzima ulikuwa ni kufukuzana tu. Ukisikia mama anaita jina lako mara ya kwanza, unajifanya husikii; likiitwa mara ya pili, unajibu “Nakuja!” lakini unaendelea kucheza. Likifika la tatu, sasa unakimbia kweli si kwa sababu umechoka kucheza, bali kwa sababu unajua ukichelewa utachezea fimbo.
Halafu kulikuwa na ile furaha ya kupewa chenji ya dukani ubaki na kiasi kidogo, kula chakula cha sikukuu, au kuambiwa kesho hakuna shule. Hatukuwa na simu za kutuburudisha, lakini tulijua namna ya kufanya siku nzima ipite bila kuchoka.