Kizazi cha 1980s ndiyo Kizazi cha Dhahabu

Kizazi cha 1980s ndiyo Kizazi cha Dhahabu

JosephNyaga

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
291
Reaction score
232
Umezaliwa lini? Baada ya 1995? Basi kuna mambo matamu ulipishana nayo. Pole.

Kizazi cha 80s ndicho kizazi kilichoshuhudia mwisho na mwanzo wa mambo mengi. Watoto wa 80s ni wale waliozaliwa mwishoni mwa 70s mpaka mwishoni mwa 80s. Ndicho kizazi kilichozaliwa katikati ya mpito wa mabadiliko ya vitu vingi.

Kwenye teknolojia hawa jamaa utoto wao wameishi kianalojia na utoto wao huo huo wameishi kidijitali. Hawa waliozaliwa miaka ya 80s huwadanganyi kitu kwa sababu wameishi maisha ya namna zote 2 na wana mengi ya kuelezea.

Utoto wao walipeleka ujumbe wa mbali kwa miguu na utoto wao huo huo ndiyo waliyo zipokea simu za mkononi kwa mara ya kwanza na kuanza kutuma ujumbe wa mbali. Hawa walilelewa na kukuzwa kwa mziki mzuri na wakashuhudia pia mwanzo wa mziki wa hovyo mziki takataka unaopigwa mpaka sasa.

Hawakuzaliwa kwenye utandawazi lakini wameukaribisha na kuuishi huo utandawazi. Hawa ndiyo watumiaji wa kwanza kabisa wa internet cafe, email, Google, Yahoo, Gmail, Hotmail na MSN. Ni mengi mno naweza kuyasema wacha nisiwamalizie nafasi ya kutiririka zaidi.

Karibuni.
 
Yes i am among 80s yani ni kizazi cha mwanzo na sasa kati nasubiri mwisho kwenye miaka ya 2050s
Hamna lolote nyie. Ndo kizazi cha hovyo kabisa. Wakati wenu hali ya dunia kila kitu kilikuwa rahis. Kwaanzia uchumi hata hali ya hewa tabia nchi.

Mkashindwa hata kutakake advantage ya kujenga nchi kama wengine waliozaliwa miaka iyo nchi zingine.

Mmetuangusha sana mliozaliowa 70s na 80s. Bure kabisa
 
Zote mkuu. Miaka ya 80s maana yake ni 1970 mpaka 1990.
Wote tu ni reject. Mngekuwa makini mliozaliwa miaka iyo taifa letu sasa hivi lisingekuwa la hovyo. Mlikuwa mpompo tu.

Hali ya maisha imekuwa ngumu kwa ajili yenu. Wakati wenu kila kitu kilikuwa rahis at your own disposal. Mkashindwa kujenga misingi thabit kwa vizazi vijavyo.
 
Maofisini nao magoroko tu kama wa 70s na 60s
 
Back
Top Bottom