Kizazi cha 2000 kitazalisha mabilionea wengi zaidi nchini kuliko waliowatangulia

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Wakati mwingine mafanikio ya mtu ni bahati ya ulizaliwa kipindi gani.

Mnawaita watoto wa 2000 ila nikwambie ndio kizazi bora kabisa kuwahi kutokea nchini. Kizazi kinajiamini sana, kukuta mtoto anamhoji mzazi wake kwa mambo ya msingi ni kawaida.

Tuendelee... Zahir Ali Zoro ana kipaji kuliko mwanae Banana,lakini kimafanikio mtoto kamuacha mbali sana baba, maana baba alizaliwa na kukua kipindi muziki ukiwa ni amature haulipi, Kuna wasanii wengi wa bongo flavor ukiwaangalia unasema hawa wangezaliwa zamani wangekuwa vibaka tu. Neymar angezaliwa miaka kumi mbele angetwaa ballon dor bahati mbaya kaanza kushine Messi na Ronaldo wako fire.

Watoto wa 2000 wamezaliwa kipindi dunia iko katika mageuzi makubwa sana ya technology. Huitaji kulima sana au kusoma sana ili utajirike, ni ujanja ujanja wako tu. Zamani wazazi wetu walifanya kazi kwa bidii mashambani na kutusihi tusome sana ili tufanikiwe, kizazi hiki hayo hayapo.

Hali hii iliwakuta wazungu miaka ya nyuma, waliheshimu kipaji kuliko vyeti vya darasani, Bill Gates ni college dropout, Ronaldo hata sijui kama alifika secondary, Beckham hata kuandika sijui kama anajua.
Tutegemee mabilione wengi toka kwa watoto wa 2000.

Kumbuka ili uendelee unahitaji, discipline, confidence, bahati na kujua kutumia fursa zilizopo kwa wakati huo.​
 
Wa huko Dar es salaam ila Mimi wa hapa kijijini hawawezi kunizidi chochote na haitotokea maana kama nakunywa nao ulanzi wananza kuongea pumba na Mimi naongea madini watanizidi nini hawa ?

Hawa ambao nawaibia vibuku ten vyao vya kahawa kwa kuwainstalia whatsapp na Facebook ?

Wa huko mjini labda ila wa hapa kijijini nimejihakikisha utawala wangu labda wanifukuze kijijini kwao
 
unawalinganisha na kizazi kipi ili kupata huo ubora wao
 
kabisa si tanzania tu hata mbele.
Siku hizi ni rahisi kutoka bila kuwa na lebo au kuhustle. mtu anaweza weka anaimba tiktok wimbo wake ukaenda viral akawa maarufu over night.
vijana wengi tanzania wametokea instagram kisanaa katika uchekeshaji wakati zamani ilibidi mpaka uitwe kaole watu wakuone kwa itv.
lakini pia ni kizazi ambacho baadaye huenda kikaanguka kwa speed ya 5G
 
Kwa vipi kinaweza kuanguka?
 
Zamani ndo watu wangefanikiwa kuzidi sasa hivi

Vijana wa 2000s wanamaliza Elimu Ila no employment opportunity while watu waliozaliwa zamani everything was there.

Kitu kikubwa kinachowafanya watoto wa 2000s wawe smart ,ambitious and focused ni scarcity they don't want to play with any opportunity.

Zamani MTU aliyekuwa Ana 30 na ni educated and smart kumkuta yupo broke .

Utandawazi upo juu Ila everything is all about trending and not insight.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…