Kizazi cha 2000 kitazalisha mabilionea wengi zaidi nchini kuliko waliowatangulia

Kizazi cha 2000 kitazalisha mabilionea wengi zaidi nchini kuliko waliowatangulia

Walifanya sehemu yao mkuu hivyo hivyo. Burudani tulipata kivyetu vyetu.
Kuna bendi ikiitwa tancut almasi ya iringa enzi za akina kasaloo kyanga,kyanga songa na john kitine,bendi ina wanamuziki zaidi ya 30,mtagawana sh ngapi hapo,TP Ok Jazz ilukuwa na vyombo Tani 20 na wanamuziki lundo,siku hizi unaingia mwenyewe studio unatoa hitsong unatupia mtandaoni tayari umetoboa
 
"Papaa ee, tutunzeeee, tutunzeeee" Unadhani anaimba kikongo kumbe mnaambiwa mumtunze fedha.
 
Wa huko Dar es salaam ila Mimi wa hapa kijijini hawawezi kunizidi chochote na haitotokea maana kama nakunywa nao ulanzi wananza kuongea pumba na Mimi naongea madini watanizidi nini hawa ?

Hawa ambao nawaibia vibuku ten vyao vya kahawa kwa kuwainstalia whatsapp na Facebook ?

Wa huko mjini labda ila wa hapa kijijini nimejihakikisha utawala wangu labda wanifukuze kijijini kwao
Yaani wewe muhenga umintallie watsapp mtoto wa 2000? Umetisha,hivi vitoto vinajua sana kuchezea simu na computer
 
Mafanikio Yanakuja kwa kumtanguliza mungu na kufanya kazi kwa bidii hamna ubilionea unakuja kwa drama acha kuwadanganya watu
Kama ingekuwa hivyo wanawake wa vijijini wangekuwa mabilionea,wanafanya sana kazi kwa bidii.kuhusu Mungu imekaa kiimani zaidi ndio nikaweka point ya bahati.
Trust me bidii bila bahati utaishia kukongoroka tu hakuna kitu utapata,confidence,nidhamu,na time and space,ulikuwa wapi muda fulani na ulikuwa unafanya nini kwa muda huo,swala la bidiii ni dogo sana,mtoto wa Ronaldo kafanya bidii gani,kuna waarabu wanavisima vya mafuta wanakunywa kahawa tu a ni mabilionea
 
Maisha ya bahati yalikuwa zamani Karne hii maisha yamebadilika Cha kwanza ukute kwenu Kuna mifumo ya maisha mazuri uyaendeleze lakini ubilionea kwa kuanza wewe mwenyewe ni ndoto za alinacha hao unaowataja walikuwa tayari mungu alishawapitisha kuwa bilionea pesa sio nywele kila mtu anazo
 
Wakati mwingine mafanikio ya mtu ni bahati ya ulizaliwa kipindi gani.

Mnawaita watoto wa 2000 ila nikwambie ndio kizazi bora kabisa kuwahi kutokea nchini. Kizazi kinajiamini sana, kukuta mtoto anamhoji mzazi wake kwa mambo ya msingi ni kawaida.

Tuendelee... Zahir Ali Zoro ana kipaji kuliko mwanae Banana,lakini kimafanikio mtoto kamuacha mbali sana baba, maana baba alizaliwa na kukua kipindi muziki ukiwa ni amature haulipi, Kuna wasanii wengi wa bongo flavor ukiwaangalia unasema hawa wangezaliwa zamani wangekuwa vibaka tu. Neymar angezaliwa miaka kumi mbele angetwaa ballon dor bahati mbaya kaanza kushine Messi na Ronaldo wako fire.

Watoto wa 2000 wamezaliwa kipindi dunia iko katika mageuzi makubwa sana ya technology. Huitaji kulima sana au kusoma sana ili utajirike, ni ujanja ujanja wako tu. Zamani wazazi wetu walifanya kazi kwa bidii mashambani na kutusihi tusome sana ili tufanikiwe, kizazi hiki hayo hayapo.

Hali hii iliwakuta wazungu miaka ya nyuma, waliheshimu kipaji kuliko vyeti vya darasani, Bill Gates ni college dropout, Ronaldo hata sijui kama alifika secondary, Beckham hata kuandika sijui kama anajua.
Tutegemee mabilione wengi toka kwa watoto wa 2000.

Kumbuka ili uendelee unahitaji, discipline, confidence, bahati na kujua kutumia fursa zilizopo kwa wakati huo.​
Ulivyo sema Beckham unahis hata kuandika hajui Uzi wako umeutia doa
 
At
Maisha ya bahati yalikuwa zamani Karne hii maisha yamebadilika Cha kwanza ukute kwenu Kuna mifumo ya maisha mazuri uyaendeleze lakini ubilionea kwa kuanza wewe mwenyewe ni ndoto za alinacha hao unaowataja walikuwa tayari mungu alishawapitisha kuwa bilionea pesa sio nywele kila mtu anazo
Bahati hazijawahi kuwana kikomo,hata kuzaluwa familia bora ni bahati ,maana si kwa juhudi zako
 
Back
Top Bottom