Njemba Soro.
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 3,732
- 6,561
watu kama wewe ni wale mliopitwa na wakati. Kwamba lazima kanuni igunduliwe hapa? Hujui kwamba yale yaliyogunduliwa tayari tunapaswa kujifunza? Nilisoma PCB na sasa napasua watu mafuvu, kama nisingejifunza kanuni zilizopo tayari nisubiri za ccm ingekuwaje? JIONGEZE ARIFU.Mathematics generation refers to the process of creating new mathematical ideas, concepts, theorems, formulas, or models. It involves exploring mathematical
Hebu niambie formula, concept,theory na models zilizogunduliwa hapa bongo ili tujue kweli wewe unaelewa ulichoanzishia uzi
sema tu ukweli ilikuwa DSafi sana mkuu, mi nilipataga C ,ila nilikua na A za chemistry, Language na Biology
Hio C hapo ndo nimefaulu yaani 😂😂😂😂
Acha ubishi mkuu, nikuoneshe cheti, au nikipe index np u google??sema tu ukweli ilikuwa D
Mbona C ni ushindi tosha kwa ugumu wa lile somo
natania rafikiAcha ubishi mkuu, nikuoneshe cheti, au nikipe index np u google??
we ndio bwege kabisa, ulitegemea impact gani. Unajua maana ya Hisabati kweli? Inatumika wapi.SAHIHISHO:Tanzania hakujawahi kuwa na kizazi Cha mathematics.
hao ni wazee wa kukariri ndo maana hakuna impact ya aina yeyote
neno bwege hukupaswa kuliwekawe ndio bwege kabisa, ulitegemea impact gani. Unajua maana ya Hisabati kweli? Inatumika wapi.
Safi sana mkuu [emoji123]Kwa kuwawekea multiple choices kwenye mitihani ya Hisabati wao(NECTA) husahihisha kwa haraka sana.
Necta wamewekeza zaidi kwenye kupunguza gharama za usahihishaji kwa kisingizio cha teknolojia.
Huenda kuna lijitu limoja kutokana na nafasi liliyokuwa nayo pale necta limewashawishi maafisa wenziwe hata hilo likapita bila kujali uhalisia wa madhara ya hilo walilolipitisha.
Kwa kidato cha 4 nao wanaruhusiwa kutumia calculator kwenye mitihani yao ilihali kwenye mihtasari wanafundishwa kutumia mathematical tables tu.
Kwa akili za watoto wanaona wamerahisishiwa ilhali hawajui kuzitumia hizo calcalator zenyewe, maana hakuna mada wanayofundishwa kuzitumia.
NECTA na TIE ni kama vile hawawasiliani ili kujenga, pengine kila mmoja anajiona mwamba na anapaswa kusikilizwa.
Unajua maana ya generation kwenye mathematics,watu kama wewe ni wale mliopitwa na wakati. Kwamba lazima kanuni igunduliwe hapa? Hujui kwamba yale yaliyogunduliwa tayari tunapaswa kujifunza? Nilisoma PCB na sasa napasua watu mafuvu, kama nisingejifunza kanuni zilizopo tayari nisubiri za ccm ingekuwaje? JIONGEZE ARIFU.
Maths unakariri?SAHIHISHO:Tanzania hakujawahi kuwa na kizazi Cha mathematics.
hao ni wazee wa kukariri ndo maana hakuna impact ya aina yeyote
Sabato NjemaI hate M. A. T. H [emoji58][emoji58]
Mleta mada hajui alicholeta hapa,anadhani hapa ni Facebook,ukikutana na watu makini lazima ukimbie Uzi na uanze matusiKwa kuwawekea multiple choices kwenye mitihani ya Hisabati wao(NECTA) husahihisha kwa haraka sana.
Necta wamewekeza zaidi kwenye kupunguza gharama za usahihishaji kwa kisingizio cha teknolojia.
Huenda kuna lijitu limoja kutokana na nafasi liliyokuwa nayo pale necta limewashawishi maafisa wenziwe hata hilo likapita bila kujali uhalisia wa madhara ya hilo walilolipitisha.
Kwa kidato cha 4 nao wanaruhusiwa kutumia calculator kwenye mitihani yao ilihali kwenye mihtasari wanafundishwa kutumia mathematical tables tu.
Kwa akili za watoto wanaona wamerahisishiwa ilhali hawajui kuzitumia hizo calcalator zenyewe, maana hakuna mada wanayofundishwa kuzitumia.
NECTA na TIE ni kama vile hawawasiliani ili kujenga, pengine kila mmoja anajiona mwamba na anapaswa kusikilizwa.
Afu wewe ni mwalimuHesabu inamsaidia Nini mtu?
Unabidi kujua
Kutoa
Kujumlisha
Kuzidisha
Kugawanya
Hadi leo?Kila mtoto anakuja na sahani yake, Math haijawai nipenda although waga nastruggle nipate good grade
Kwamba ile shule ya wahaya ina madarasa 12?Mimi nilipata A mwaka 2010 darasa la 12 so I wish watu wangepambana hesabu za pesa huko shuleni kuliko za darasani.
uongo kabisa huu mr ngoja nikuoneshe maswali mojawapo ya mwaka jana 2022 watoto wako deep sana ila inategemea na shule kama kidumu na mfagio wachache ila magari ya njano wanazibonda sana HesabuKila nikimkumbuka mwalimu wangu wa Hisabati Mwalimu Msiagi alivyokuwa akitujengea confidence katika somo la Hisabati zikiwemo test za asubuhi pamoja na kuielewa table na kuiweka kichwani hakika ilitujenga sana.
Lakini Sasa mtaala umebadilisha kuwa mitihani ya hesabu shule ya msingi Wanachagua yaani tayali wamewekewa majibu kabisa.
Mfano 3+4 (a) 2 (b) 4 (c) 7.
Huu mfumo umetengeneza vijana wavivu sana, wanafunzi hawataki kufikiria kabisa pamoja na kukokotoa anachokifanya ni kufumba macho na kuotea tu.
Msingi wa mtoto kupenda hesabu ni kuanzia chini kabisa yaani shule ya msingi ule mfumo wa mwanzo ulikua Bora sana tofauti na mfumo wa Sasa maana umetengeneza kizazi Cha kubashiri (kubeti).
Hivi Sasa ukikagua mitihani ya mtoto haswa ya hesabu unakuta swali Fulani kapata lakini swali Hilo Hilo ukimwambia alifanye kwa njia hawezi hata kidogo kumbe yeye aliotea tu na kwa kuwa ni bingwa wa kuotea basi anaonekana Bora mbele ya wale wasiokuwa Bora katika zoezi la kubashiri.
Mfumo wa Zamani ukikutana na kipanga wa Hisabati anakuwa ni kipanga kweli kweli lakini hivi Sasa kwa shule ya msingi kutokana na huo mfumo wakuchagua naona kabisa kizazi Cha Hisabati kinapotea taratibu kinabaki kizazi Cha kubeti.
Ombi langu kwa Wizara ya Elimu iangalie upya huu mtaala wa shule ya msingi haswa somo la Hisabati wafute huo muundo wa kuchagua ili kunusuru kizazi Cha Hisabati (mathematics)
Nawasilisha hoja.
Mbona unajitekenya halafu unacheka??uongo kabisa huu mr ngoja nikuoneshe maswali mojawapo ya mwaka jana 2022 watoto wako deep sana ila inategemea na shule kama kidumu na mfagio wachache ila magari ya njano wanazibonda sana Hesabu
we umesema mtihani mwepesi wa hesabu mi nimekataaMbona unajitekenya halafu unacheka??
Asilimia 90 ya Watoto wa Tanzania wanasoma shule gani???
Ongea fikra huruAfu wewe ni mwalimu