Kizungu, Kizungumkuti na kizunguzungu!

Kizungu, Kizungumkuti na kizunguzungu!

Heshima yenu wakubwa Kwa wadogo.

Nina swali gumu sana naomba mnijibuni.
Kwa anayejua PIKIPIKI kwa KIZUNGU inaitwaje naomba anisaidie.
Atakaeleta jibu sahihi zawadi yake ni vocha ya Tsh 10,000/= ( elfu kumi tu).
Asanteni sana.
Honey of beauties
 
Motorbike.
NB;Usitume hiyo vocha ya kilimo kwanza. Tutumie wote ada aliyotoa baba yangu kueneza upendo.
 
Ahaha tupe jibu basi
Motorcycle ina majina haya
1. Scooter
2. BIKE
3. Motor Bike

Wewe unayakataa wakati hujui, tupe majibu
Scooter,BIKE na motor Bike siyo maneno ya kizungu hayo, yaani hapo Baado hujasema! Swali hili ni chemsha bongo tu na nilijua kuwa wengi watakosea.
Waliojibu kuwa "hakuna lugha inaitwa kizungu" wamepatia ila hawawezi pata vocha kwa sababu wamejibu swali ambalo hawajaulizwa!!!!!!.
Swali ni taja "pikipiki kwa kizungu inaitwaje?! Jawabu ni kwamba duniani hakuna lugha inayoitwa " KIZUNGU" Jawabu ni sahihi ila siyo la swali lililoulizwa kwahiyo aliyejibu nampa congratulation lakini vocha ataendelea kusubiri.
 
Wazungu wapo
Waczech
Waitali
Wahispania
Waholanzi
Wareno
Waingereza
Hakuna lugha za kizungu
Safi sana! Hizo ni lugha za watu wa bara la ulaya ambao kwa kiswahili wanaoitwa WAZUNGU ambao wanaongea lugha tafauti lakini hakuna lugha Moja inayoitwa KIZUNGU.
Swali lilikuwa CHEMSHA BONGO kupima uelewa wa watu na wewe KALAGA BAGO NONGWA umelielewa na kutoa jibu sahihi japo sio la swali uliloulizwa kwahiyo nasema congratulation.
 
Kwa hiyo shiling kumi yangu naipata mkuu? Nimekuachia namba hapo inbox. Nitakuja kutoa shuhuda hapa na screenshot ya malipo! Woooooooyooooooo!
 
Back
Top Bottom