Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.
Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.
Sakata la Dowans: ICC Siyo Mahakama wala ya Kijiji licha ya Kimataifa
Mimi nawashangaa Watz wengi, tena walioenda shule, wanavyochukulia vitu kijuu juu tu bila uchambuzi na kupokea wanayoambiwa tu bila kuyachekecha. Watu wanasema kuna mahakama ya kimataifa imehukumu kuwa Dowans walipwe billion 185 na serikali ya Tz. Mara moja hoja ikawa tulipe au tusilipe? Kumbe swali la ukweli wa hayo maamuzi na nguvu zake kisheria vikasahaulika. Hata baada ya serikali kuchakachua hiyo "hukumu" na kuamua kulipa nusu tu ya hizo hela bado watu wengine hawajashtuka. Mahakama gani hiyo ambayo mhukumiwa anaamua mwenyewe kujirekebishia adhabu yake?
Kwanza ICC kirefu chake ni International Chamber of Commerce. Yaani ni taasisi ya kiraia kama NGO hizi za kwetu. Haina uwezo wa kuwa mahakama kwani mahakama ni chombo cha sheria na hivyo kokote duniani ni chombo cha serikali. Kitu ICC ilicho nacho ni kitengo cha arbitration, ambacho kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili ni kitengo cha Usuluhishi na siyo mahakama. Kwa kuwa ICC ni taasisi ya kiraia hiki kitengo cha usuluhishi ni cha hiari kabisa: pande zote mbili zinakubaliana kuhusu ni nani awe msuluhishi na ni mambo gani ya kusuluhisha, ni wapi watakaa, lini na kwa muda gani?.
Sasa kwa kuwa katika swala la Dowans viongozi wa serikali na Dowans walikuwa upande mmoja, hakukuweko na tatizo lolote kati ya upande ulioitwa wa serikali na upande ulioitwa wa Dowans kwa hiyo mambo yote watakuwa walikubaliana. Swali lililokuweko ni kudanganya wananchi kuwa kumekuweko na hukumu ya mahakama ya kimataifa na serikali inatakiwa kutekeleza hiyo hukumu ...
Majibu ya maswali yote hayo ni ndio. Mitambo ipo wapi? NDIO.
Ilizalisha umeme haikuzalisha? NDIO.
Huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? NDIO.
Mkataba ulivunjwa kabla ya muda? NDIO.
DUUUUUH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Gbrain usilete habari za kizushi,tutajie huyo board member ni nani
Huyu Genius barin ametoka shule ya kata, walimu wawili, wanafunzi 180. face to face na mwalimu wake ajawai fanya. Anashida sana. He lacks creative thinking. due to lact of intuitive mind
Unataka kuendeleza maneno maneno maneno tuu kama tulivyo watanzania badala ya kukazana kutafuta mbinu za kujikwamua kwenye umaskini munatupotezea na dowans ili tusahau kama kura mulichakachua,mumeshindwa kutawala nchi,mumeingiza nchi kwenye fedheha kuu,kama munadhani watanzania ni walewale wa kusahau mumeunywa,senti tano haitoki na mkilazimisha mutaipata
Watanzania tunapumbazwa akili zetu hadi tunasahau kama kuna mgao wa umeme, DOWANS is just a HOAX, GeniusBrain kaamua kuchukua hayo aliyoambiwa na mjumbe wa bodi na kuamini kila kitu, sasa labda nimuulize tu what makes him think kwamba huyo mjumbe wa bodi anayoyaongea ni kweli? Na kama kulipa deni kwanini Tanesco wasilipe kwa hela zao wenyewe na badala yake waanze kutupandishia sisi watumiaji wa umeme ili waweze kufidia deni kuna vitu vingine you don't need to do maths.
Mimi nataka kujua ni nani alisaini huo mkataba hapo ndipo tunaanzia
Mkuu GeniusBrain we wamekuahidi asilimia ngapi (%) kwa kuleta hizi pumba hapa?!!!!
Mh GeniusBrain umetumwa au?
Hivi ukitazama mtiririko mzima kuna mahala unaridhika ya kuwa Dowans ni halali eeeeTanesco ni shirika la nani kwani ? wewe hata muundo huujui kumbe tukusaidiaje sijui
Sakata la Dowans: ICC Siyo Mahakama wala ya Kijiji licha ya Kimataifa
Mimi nawashangaa Watz wengi, tena walioenda shule, wanavyochukulia vitu kijuu juu tu bila uchambuzi na kupokea wanayoambiwa tu bila kuyachekecha. Watu wanasema kuna mahakama ya kimataifa imehukumu kuwa Dowans walipwe billion 185 na serikali ya Tz. Mara moja hoja ikawa tulipe au tusilipe? Kumbe swali la ukweli wa hayo maamuzi na nguvu zake kisheria vikasahaulika. Hata baada ya serikali kuchakachua hiyo "hukumu" na kuamua kulipa nusu tu ya hizo hela bado watu wengine hawajashtuka. Mahakama gani hiyo ambayo mhukumiwa anaamua mwenyewe kujirekebishia adhabu yake?
Kwanza ICC kirefu chake ni International Chamber of Commerce. Yaani ni taasisi ya kiraia kama NGO hizi za kwetu. Haina uwezo wa kuwa mahakama kwani mahakama ni chombo cha sheria na hivyo kokote duniani ni chombo cha serikali. Kitu ICC ilicho nacho ni kitengo cha arbitration, ambacho kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili ni kitengo cha Usuluhishi na siyo mahakama. Kwa kuwa ICC ni taasisi ya kiraia hiki kitengo cha usuluhishi ni cha hiari kabisa: pande zote mbili zinakubaliana kuhusu ni nani awe msuluhishi na ni mambo gani ya kusuluhisha, ni wapi watakaa, lini na kwa muda gani?.
Sasa kwa kuwa katika swala la Dowans viongozi wa serikali na Dowans walikuwa upande mmoja, hakukuweko na tatizo lolote kati ya upande ulioitwa wa serikali na upande ulioitwa wa Dowans kwa hiyo mambo yote watakuwa walikubaliana. Swali lililokuweko ni kudanganya wananchi kuwa kumekuweko na hukumu ya mahakama ya kimataifa na serikali inatakiwa kutekeleza hiyo hukumu ...
JF, home of great thinkers. There once a time was a great thinker called Malaria Sugu. He died and on the third day he rose again with a genius brain.Nimewaambia kile ambacho ni ukweli, walipwe dowans pesa zao kwani ni halali yao kwa umeme wao walio tuzalishia na tukautumia
Hivi ukitazama mtiririko mzima kuna mahala unaridhika ya kuwa Dowans ni halali eeee
JF, home of great thinkers. There once a time was a great thinker called Malaria Sugu. He died and on the third day he rose again with a genius brain.