Kizungumkuti Dowans

Kizungumkuti Dowans

Majibu ya maswali yote hayo ni ndio. Mitambo ipo wapi? NDIO.
Ilizalisha umeme haikuzalisha? NDIO.
Huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? NDIO.
Mkataba ulivunjwa kabla ya muda? NDIO.
DUUUUUH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mimi nataka kujua ni nani alisaini huo mkataba hapo ndipo tunaanzia
 
Hya basi hayo yote sawa tuambie sasa huyo managing director wa dowans ni nani? Maana hakuna compuni isiyokuwa na mwenyewe,isiyokuwa na manager mwajiri isiyokuwa na accountant!! hii dowans haina hao wote? ama ni ya shetani

Tokea lini ukalipa kampuni ambayo haujui wamiliki wake
 
Hivi kwani wamiliki wa Richmond na Dowans waliotajwa kwenye report ya kamati ya Mwakembe ndio hao hao waliotajwa na Mh. Waziri Geresha [Ngereja] siku alipokutana na waandishi? mwenye ile riport ya Mwakembe aiweke hapa tui review.
Kumbe ndiyo anaitwa hivi siku hizi
 
Jamaa wanatunga vistori vyao , afu wanakuja kwetu kutaka tuwahalalishie!!

Nendenu zenu kuleee. Mkitaka kulipa lipeni tu...lakini msitufanye mazezeta! Wezi wakubwa!!!!
 
Jamaa wanatunga vistori vyao , afu wanakuja kwetu kutaka tuwahalalishie!!

Nendenu zenu kuleee. Mkitaka kulipa lipeni tu...lakini msitufanye mazezeta! Wezi wakubwa!!!!

Hii ni kama vile sinema ya kihindi starring anaonyeshwa amekufa ile picha inakaribia kuisha wanamuonyesha akiwa yu hai
 
Binafsi nafikiri ni wakati wa Mkuu wa Nchi kuzungumza kuhusu suala hili, kwani hata bunge lenyewe halina ubavu tena chini ya Spika Anne. Kesho atakuja hapa mtu mwingine na kusema kakutana na Lowassa Monduli kamwambia Dowans ni mali ya Sophia Simba.

Huku kesho yake mwingine atakutana na Zitto Kabwe na atamwambia yeye (Zitto) kama Mwenyekiti wa Hesabu za Mashirika ya umma likiwemo Tanesco ndo anajua Dowans wanatakiwa kulipwa.

Mwishowe tutajikuta tunapoteza muda tu!!

Mkuu Ukweli wa Dowans unajulikana tangu hapo nyuma, ni vile kuna watu wengine kazi yao ni kutetea tu, na wanatetea kwa misingi yao binafsi
 
Duuh makubwa ahsante kwa kutupa taarifa inayosaidia kuthibitisha kwamba swala la Dowans ni mchoro wa wakubwa serikalini
 
wanaogopa bunge, wameshafanya kabla bunge halijaanza. nasikitika kusikia hivyo. hivyo hata kama wabunge watapiga kelele sana, pesa imeshaenda, na hakuna kitakachobadilisha walichokifanya. kwani wakilipa, sisi watz tunao uwezo kuwafanya nini? si tutapiga kelele san ahalafu badaye tunanyamaza tunaletewa zengwe lingine tunaanza kulijadili na kuhangaika nalo? akianza lowasa, tunabadilishiwa zengwe anakuwa chenge, akija richmond, anakuwa kagoda, tunasahau yote, mara dowans tunasahau kagoda...etc. so wameshatujua kuwa hatuna lolote, na wengi wa wanaofanya hayo wamejaa humuhumu kwenye JF na wanachangia hata mawazo pengine....hii ndo inchi yetu.
 
sasa unahangaika nini wenzio wanasema pesa zishalipwa? tuanze tu kujadili mambo mengine, hilo tushalizwa tayari...habari ndo hiyo.
 
Sakata la Dowans: ICC Siyo Mahakama wala ya Kijiji licha ya Kimataifa

Mimi nawashangaa Watz wengi, tena walioenda shule, wanavyochukulia vitu kijuu juu tu bila uchambuzi na kupokea wanayoambiwa tu bila kuyachekecha. Watu wanasema kuna mahakama ya kimataifa imehukumu kuwa Dowans walipwe billion 185 na serikali ya Tz. Mara moja hoja ikawa tulipe au tusilipe? Kumbe swali la ukweli wa hayo maamuzi na nguvu zake kisheria vikasahaulika. Hata baada ya serikali kuchakachua hiyo "hukumu" na kuamua kulipa nusu tu ya hizo hela bado watu wengine hawajashtuka. Mahakama gani hiyo ambayo mhukumiwa anaamua mwenyewe kujirekebishia adhabu yake?

Kwanza ICC kirefu chake ni International Chamber of Commerce. Yaani ni taasisi ya kiraia kama NGO hizi za kwetu. Haina uwezo wa kuwa mahakama kwani mahakama ni chombo cha sheria na hivyo kokote duniani ni chombo cha serikali. Kitu ICC ilicho nacho ni kitengo cha arbitration, ambacho kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili ni kitengo cha Usuluhishi na siyo mahakama. Kwa kuwa ICC ni taasisi ya kiraia hiki kitengo cha usuluhishi ni cha hiari kabisa: pande zote mbili zinakubaliana kuhusu ni nani awe msuluhishi na ni mambo gani ya kusuluhisha, ni wapi watakaa, lini na kwa muda gani?.

Sasa kwa kuwa katika swala la Dowans viongozi wa serikali na Dowans walikuwa upande mmoja, hakukuweko na tatizo lolote kati ya upande ulioitwa wa serikali na upande ulioitwa wa Dowans kwa hiyo mambo yote watakuwa walikubaliana. Swali lililokuweko ni kudanganya wananchi kuwa kumekuweko na hukumu ya mahakama ya kimataifa na serikali inatakiwa kutekeleza hiyo hukumu ...

Kama ni kweli unayoyasema, basi hapo kuna mgao wa wengi kwenye serikali yetu!
 
sasa unahangaika nini wenzio wanasema pesa zishalipwa? tuanze tu kujadili mambo mengine, hilo tushalizwa tayari...habari ndo hiyo.

Una uhakika na unachokisema??!! Ninachojua iko kesi mahakamani kupinga malipo hayo...sidhani kama wataweza kufanya kinyemela!
 
Sakata la Dowans: ICC Siyo Mahakama wala ya Kijiji licha ya Kimataifa

Mimi nawashangaa Watz wengi, tena walioenda shule, wanavyochukulia vitu kijuu juu tu bila uchambuzi na kupokea wanayoambiwa tu bila kuyachekecha. Watu wanasema kuna mahakama ya kimataifa imehukumu kuwa Dowans walipwe billion 185 na serikali ya Tz. Mara moja hoja ikawa tulipe au tusilipe? Kumbe swali la ukweli wa hayo maamuzi na nguvu zake kisheria vikasahaulika. Hata baada ya serikali kuchakachua hiyo "hukumu" na kuamua kulipa nusu tu ya hizo hela bado watu wengine hawajashtuka. Mahakama gani hiyo ambayo mhukumiwa anaamua mwenyewe kujirekebishia adhabu yake?

Kwanza ICC kirefu chake ni International Chamber of Commerce. Yaani ni taasisi ya kiraia kama NGO hizi za kwetu. Haina uwezo wa kuwa mahakama kwani mahakama ni chombo cha sheria na hivyo kokote duniani ni chombo cha serikali. Kitu ICC ilicho nacho ni kitengo cha arbitration, ambacho kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili ni kitengo cha Usuluhishi na siyo mahakama. Kwa kuwa ICC ni taasisi ya kiraia hiki kitengo cha usuluhishi ni cha hiari kabisa: pande zote mbili zinakubaliana kuhusu ni nani awe msuluhishi na ni mambo gani ya kusuluhisha, ni wapi watakaa, lini na kwa muda gani?.

Sasa kwa kuwa katika swala la Dowans viongozi wa serikali na Dowans walikuwa upande mmoja, hakukuweko na tatizo lolote kati ya upande ulioitwa wa serikali na upande ulioitwa wa Dowans kwa hiyo mambo yote watakuwa walikubaliana. Swali lililokuweko ni kudanganya wananchi kuwa kumekuweko na hukumu ya mahakama ya kimataifa na serikali inatakiwa kutekeleza hiyo hukumu ...

Hoja yako kama ina mashiko. Kwa kuwa chama kinachounda serikali ndicho kilichoshika mpini wa panga, basi nakushauri uangane na kada wao Mh. Nimrodi Mkono kuandaa hoja za kukwepesha malipo haya. Hata hiyo sina hakika kama Nimrodi kweli ana dhamira ya thati ya kulisaidia taifa liondokane na mzigo huu au ilikuwa ni danganya toto tuu
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.
Mkuu GeniusBrain we wamekuahidi asilimia ngapi (%) kwa kuleta hizi pumba hapa?!!!!
 
If it's true then it's quite amazing and I will kick myself for not thinking that!! Good Stuff man!
 
Unataka kuendeleza maneno maneno maneno tuu kama tulivyo watanzania badala ya kukazana kutafuta mbinu za kujikwamua kwenye umaskini munatupotezea na dowans ili tusahau kama kura mulichakachua,mumeshindwa kutawala nchi,mumeingiza nchi kwenye fedheha kuu,kama munadhani watanzania ni walewale wa kusahau mumeunywa,senti tano haitoki na mkilazimisha mutaipata
 
Huyu Genius barin ametoka shule ya kata, walimu wawili, wanafunzi 180. face to face na mwalimu wake ajawai fanya. Anashida sana. He lacks creative thinking. due to lact of intuitive mind
 
Back
Top Bottom