Kizungumkuti Dowans

Kizungumkuti Dowans

Habari nilizozipata usiku wa jana ambazo ni za kweli ni kwamba dowans wameshalipwa,kwa ufupi watanzania tumeshapigwa changa la macho.na nyie wadau fuatilieni mpate taarifa zaidi,Ila kwa upande wangu taarifa hizi nimezipata kupitia mtu wa karibu sana na mmoaja ya wakurugenzi ndani ya shirika mwenye uchungu na yaliyojiri.
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Iko danganya toto tanzania eeeeh!

Mbona katika kipindi chote hicho hawakusema vitu hivyo ambavyo vilikuwa straight forward wanakuja kuzungumza sasa katika saa za majeruhi?
 
habari nilizozipata usiku wa jana ambazo ni za kweli ni kwamba dowans wameshalipwa,kwa ufupi watanzania tumeshapigwa changa la macho.na nyie wadau fuatilieni mpate taarifa zaidi,ila kwa upande wangu taarifa hizi nimezipata kupitia mtu wa karibu sana na mmoaja ya wakurugenzi ndani ya shirika mwenye uchungu na yaliyojiri.

sitaki kuamini.
 
aaaaaaaah wapi? zimetoka account gani hizo fedha?
 
Sakata la Dowans: ICC Siyo Mahakama wala ya Kijiji licha ya Kimataifa

Mimi nawashangaa Watz wengi, tena walioenda shule, wanavyochukulia vitu kijuu juu tu bila uchambuzi na kupokea wanayoambiwa tu bila kuyachekecha. Watu wanasema kuna mahakama ya kimataifa imehukumu kuwa Dowans walipwe billion 185 na serikali ya Tz. Mara moja hoja ikawa tulipe au tusilipe? Kumbe swali la ukweli wa hayo maamuzi na nguvu zake kisheria vikasahaulika. Hata baada ya serikali kuchakachua hiyo “hukumu” na kuamua kulipa nusu tu ya hizo hela bado watu wengine hawajashtuka. Mahakama gani hiyo ambayo mhukumiwa anaamua mwenyewe kujirekebishia adhabu yake?

Kwanza ICC kirefu chake ni International Chamber of Commerce. Yaani ni taasisi ya kiraia kama NGO hizi za kwetu. Haina uwezo wa kuwa mahakama kwani mahakama ni chombo cha sheria na hivyo kokote duniani ni chombo cha serikali. Kitu ICC ilicho nacho ni kitengo cha arbitration, ambacho kwa tafsiri sahihi ya Kiswahili ni kitengo cha Usuluhishi na siyo mahakama. Kwa kuwa ICC ni taasisi ya kiraia hiki kitengo cha usuluhishi ni cha hiari kabisa: pande zote mbili zinakubaliana kuhusu ni nani awe msuluhishi na ni mambo gani ya kusuluhisha, ni wapi watakaa, lini na kwa muda gani?.

Sasa kwa kuwa katika swala la Dowans viongozi wa serikali na Dowans walikuwa upande mmoja, hakukuweko na tatizo lolote kati ya upande ulioitwa wa serikali na upande ulioitwa wa Dowans kwa hiyo mambo yote watakuwa walikubaliana. Swali lililokuweko ni kudanganya wananchi kuwa kumekuweko na hukumu ya mahakama ya kimataifa na serikali inatakiwa kutekeleza hiyo hukumu ...
 
Habari nilizozipata usiku wa jana ambazo ni za kweli ni kwamba dowans wameshalipwa,kwa ufupi watanzania tumeshapigwa changa la macho.na nyie wadau fuatilieni mpate taarifa zaidi,Ila kwa upande wangu taarifa hizi nimezipata kupitia mtu wa karibu sana na mmoaja ya wakurugenzi ndani ya shirika mwenye uchungu na yaliyojiri.

Pumba tupu!
 
Jana kwenye pita pita yangu nilikutana na Mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco. Katika maongezi nae nilimuulizia kuhusu suala la Dowans. Kwenye maelezo yake ni kuwa malipo ya Dowans ni halali kabisa, kwani wanacho kidai ni gharama za umeme ambao wao walizalisha na hawakuwahi kulipwa na Tanesco mpaka mkataba pale ulipo vunjwa.
Kwa maana hiyo basi, wanadai hela yao halali kabisa ambayo umeme ulizalishwa na mie na wewe tuliutumia. Sasa hapo malipo ambayo sio halali ni yepi ? au tuna nia ya kudhulumu haki za watu ?.

Na kuhusu hukumu ya mahakama ya ICC wao vitu walivyo uliza ni vichache tu, kama mitambo ipo wapi ? ilizalisha umeme au haikuzalisha ? huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? Mkataba ulivunjwa kabla ya muda ?. Majibu ya maswali yote hayo ni ndio, ndipo mahakama ikatoa huku ya Dowans kulipwa haki yao kwa kile walichotuzalishia na kukitumia.

Unataka kupima uwezo wa kufikiri wa wana jf siyo? We ni Rostam Aziz mwenyewe-we are aware of that!
 
jamani inawezekana, Jamaa keshasema source yake nadhani cha muhimu ni kufuatilia na kujua huo ukweli, mimi ndio naanza kufuatilia sasa
 
Kama wamelipwa kweli, na sio tetesi basi kwa mbali ninaweza kuamini zile thread zilizokuja karibuni zikisema kuwa hazina hakuna kitu, hazina imekauka!
TRA watakusanya nyengine kwa ajili ya kuilipa ile kampuni itakayoinunua Dowans. Mduara!
 
Hya basi hayo yote sawa tuambie sasa huyo managing director wa dowans ni nani? Maana hakuna compuni isiyokuwa na mwenyewe,isiyokuwa na manager mwajiri isiyokuwa na accountant!! hii dowans haina hao wote? ama ni ya shetani
 
Majibu ya maswali yote hayo ni ndio. Mitambo ipo wapi? NDIO.
Ilizalisha umeme haikuzalisha? NDIO.
Huko nyuma walikuwa wanawalipa au hawakuwalipa? NDIO.
Mkataba ulivunjwa kabla ya muda? NDIO.
DUUUUUH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kumbe inawezekana kutunga ka-stori ili kaendane na mtazamo wako eeh? Nilikuwa sijui hiyo...
 
Hivi kwani wamiliki wa Richmond na Dowans waliotajwa kwenye report ya kamati ya Mwakembe ndio hao hao waliotajwa na Mh. Waziri Geresha [Ngereja] siku alipokutana na waandishi? mwenye ile riport ya Mwakembe aiweke hapa tui review.
 
Kumbe siku zoote unabishana bishana hapa na kupotezea watu mida hata hufahamu kinachoongelewa ni nini na kinachodaiwa nni nini. Shame on you!!!!

Kiongozi umenifurahisha sana!

Hawa jamaa wanataka kutuzuga..hiyo mikataba..ilisaiwa fasta fasta na mze wa Monduli bila kufuata procedures. SASA LEO TUNAAMBIWA TULIPE. Hivi hawa jamaa wanatuonaje? To me its an insult kuambiwa tulipie umeme ambao hatukutumia. Now I know kwa nini nchi maskini viongozi wamekuwa kama criminal networks.

Unajua one of the charcteristics za failed states (na Africa ziko nyingi) ni viongozi kushirikiana na matapeli (transnational criminal gangs) kuwaibia wananchi. SASA NIAMBIENI KWELI KAMA KUNA TOFAUTI na viongozi wetu wanachotufanyia hapa kuhusu DOWANS na madudu mengine....
 
Watanzania tunapumbazwa akili zetu hadi tunasahau kama kuna mgao wa umeme, DOWANS is just a HOAX, GeniusBrain kaamua kuchukua hayo aliyoambiwa na mjumbe wa bodi na kuamini kila kitu, sasa labda nimuulize tu what makes him think kwamba huyo mjumbe wa bodi anayoyaongea ni kweli? Na kama kulipa deni kwanini Tanesco wasilipe kwa hela zao wenyewe na badala yake waanze kutupandishia sisi watumiaji wa umeme ili waweze kufidia deni kuna vitu vingine you don't need to do maths.
 
Back
Top Bottom