MBINU MPYA CCM KUJILIPA MARA 3 SHEA WANAYOISUBIRIA DOWANS KWA KUWAUZIA WANANCHI JOTO JINGI NA GIZA NENE KWA MAVUNO MANONO ZAIDI KARIAKOO:
Enyi wana CCM, Dowans hatuwalipi hata senti moja kutoka kwenye kodi zetu mbona hatuelewani??
Ni kero kubwa ilioje kwamba wananchi tuwashike viongozi wabadhirifu serikalini na tuhuma nzito za kutupora kwa miaka mingi kodi zetu kwa kutumiamakampuni ya kitapeli yasiojulikana wamiliki wake halafu hata bila ya jibu hilo sasa muanze kugeuza Kiswahili cha kujadilkiana na WEZI ETI KUPUNGUZIANA KIWANGO CHA FEDHA ZA WIZI WA KUWALIPA; hizi ndizo busara za wapi??
Kama hilo halitoshi, CCM hii hii bado inatuona mataahira wale wale wa miaka ya jana kwa kutuaminisha ya kwamba MTUHUMIWA WETU, NIMROD MKONO, MBUNGE MWAKILISHI WA JIMBO LA UFISADI, MFILISI WA BoT BILA UZALENDO NA MTAALAM WA KUTUFUNGISHA MIKATABA ya kuletea taifa shimanzi kila mwaka eti ndio sasa aende mahakamani kutuwakilisha katika mpango wa wizi aliouunda mwenyewe ili kwa janja za nyani tukapunguziwe kitu.
Nasema hatudanganyiki, kama AG Werema na sisi Nguvu ya Umma Jalada la Dowans tumelifunga badala yake tukutane bungeni Dodoma kwa hili ili chombo chenye mamlaka kisheria kusimamia uthibiti wa mapato na matumizi ya serikali itupe mwelekeo zaidi kwa kuzingatia kumbukumbu zilizomo ndani ya Hansard ya bunge baada ya Tume ya Mwakyembe kuwashilisha ripoti yake.
Acheni kujibaraguja hapa, kilichobakia ni sisi wananchi kutoa adhabu ya kihistoria ili ije iwe fundisho tosha kwa vyama vya kisiasa vinavyoongozwa na WALAGHAI NA MAFISADI WAKUU kama ilivyo kwa CCM. Wabunge wa CCM, kuna jambo bado wengi wenu hamjalielewa hapa; sisi wananchi hatuko kwenye mzaha na nyinyi.
Tunajua fika ni kazi gani tuliwatuma bungeni na kwamba mkienda vipi na basi iwe vipi. Katika hii kashfa na pia suala la KATIBA MPYA mchakato kuanzia bungeni sisi hesabu zetu hapo ni kwamba AMA UKO NA SISI AU UKO PAMOJA NA KAMBI YA MAFISADI ITAKAYOKUPIGIA KURA TENA HUKO MBELE YA SAFARI. Tuelewane vizuri kabisa hapo.
Naona kwenye mtego huu hata huyu ndugu tuliewahi kumuamini, Mizengo Pinda (ambaye hadi sasa kajigeuza Mtoto wa Mkulima wa Mjini) naye kajiingiza kichwa kichwa mle lakini bahati yake alishatangaza kwenda kupumzika siasa baada ya hapa, je nyinyi??
Na kwa bahati mbaya sana sana, Nguvu ya Umma uchunguzi wetu jijini umebaini kwamba kwanza mpaka sasa hivi CCM imeshajilipa zaidi ya mara 3 ya udanganyifu kwa Dowans kwa kule