Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 450
- 3,368
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Jumatatu Novemba 10.2025
Hata hivyo, tofauti na siku zote ambapo Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo huwa anafikishwa Mahakaman, lakini leo hajafikishwa Mahakamani kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama
Baada ya shauri hilo kuanza mbele ya Jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, wakili wa Serikali Mkuu Thawabu Issa ameieleza Mahakama kuwa Lissu hakufikishwa Mahakamani hapo kwa sababu za kiusalama
Hata hivyo amesema wao (Jopo la Mawakili wa Jamhuri) wametambua hilo walipofika Mahakamani na kutomkuta mshtakiwa wakalazimika kuwasiliana na Mkuu wa Magereza ambae aliwaeleza kuwa Lissu hatoweza kuletwa kwa sababu za kiusalama.
Jambo TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na kinachoendelea Mahakamani hapo kuhusiana na kesi hiyo.
Pia soma GE2025 - Jamhuri yashindwa kuleta Shahidi Mahakamani kuthibitisha Uhaini wa Lissu, kesi yaahirishwa hadi Novemba 12, 2025