KERO Kizungumkuti vyeti vya wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
Wahitimu wa Chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Upanga Dar Es Salaam wapo katika wakati mgumu baada ya chuo hicho kushindwa kuwapa vyeti vyao vya kuhitimu bila maelezo yanayoeleweka.

Hatua hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya wahitimu hao kutunukiwa shahada za umahiri na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar Dr. ALI MUHAMMED SHEIN December 5 mwaka huu katika ukumbi wa JNICC Dar Es Salaam.

Baadhi ya wahitimu wamelalamika kuwa Waajiri wao wamegoma kutambua Transcripts ambazo wamezipokea kutoka kwa wahitimu hao na hivyo kutoongeza kiasi cha mshahara kama taratibu zao za ajira zinavyotaka. Aidha baadhi ya wahitimu wamelalamika kuwa hawatapandishwa madaraja iwapo vyeti hivyo havitakuwepo.
Kinacholeta ukakasi ni ukimya wa chuo husika katika kushughulikia jambo hilo. Uongozi wa chuo haujasema lolote zaidi ya kujibu 'vikiwa tayari tutawajulisha' bila kusema ni lini vitakuwa tayari.
Wapo wahitimu waliokosa fursa ya kuendelea na masomo ya juu zaidi ya uzam8vu katika vyuo vingine sababu ta ucheleweshaji wa vyeti hivyo.

Tunawataka Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kujitokeza ku address tatizo hili na kuwaambia wahitimu ni lini watarajie kupata vyeti vyao ambavyo wametumia rasilmali zao muhimu kuhakikisha wanahitimu na hatimaye wawe na sifa stahiki za kuendelea kiuchumi na kielimu.
 
Haha! Watu wana nguvu sana na energy ya campus, yan just ndo wamegraduate washalalamika. Kwani hivyo vyeti walinyimwa au ilikuwa bado hawajakamilisha. Wawe na subira.
 
Back
Top Bottom