KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

Safi sana Askofu,hakika ww si mnafiki,Mungu ambariki Dr Bagoza,Bishop
 

Wewe acha kutapika, katika kanisa katoliki kiongozi wa ngazi ya juu ni Papa, msaidizi ni cardinal, kiutaratibu wote hawa ni maaskofu katika ngazi za juu. Maaskofu wote Tanzania wanafanya kazi chini ya cardinal anayemuwakilisha papa katika nchi.nchi huwa na kiongozi mkuu wa kanisa mmoja. Maaskofu wote wanasikiliza yeye anaelekeza nini kiutendaji.
Suala la maamuzi ta TEC cardinal anaingia kama maaskofu wengine na hivyo hutoa ushauri na kiutaratibu huwa hapaswi kutoa amri isipokuwa hushauri tu. Sasa msimpake tope kiongozi huyu kwa umamuma wenu na ushabiki wa kihuni. Aliyekuambia cardinal hasikilizwi nani.
Aliyetia ruhusa kusoma walaka kanisani ni yeye na kama kiongozi wa kanisa angeamua kupunga kannisa lisishiriki kwenye walaka hakuna mtu angeusoma kwa kuwa tu amuamini.
Askifu mkuu marasusa pua angesema hapana hakuna askofu chini yake au muumini angevutana shati na yeye. Hawa maaskofu wote wanahekima ndi maana wamewaachia waumini waelimishwe bila kulazimishwa.
 

Daaaah huyo askofu noma sana bonge la kichwa
 
Katika ibada ya pasaka iliyofanyika katika usharika wa Kayanga dayosisi ya Karagwe Baba Askofu Dr Benson Bagonza aliwatolea uvivu wavivu wa kufikiri kwa hoja zifuatazo:

1. Sisi makanisa tunapojenga shule mbona hatuambiwi tunaingilia kazi za serikali?

2. Tunapojenga miradi ya maji mbona hatuambiwi tunaingilia kazi za wizara ya maji?

3. Tupoombea mvua mbona hatuambiwi tunaingilia mamlaka ya hali ya hewa?

4. Tunaposifia serikali mbona hatulaumiwi, lakini tunapokosoa tunakaribia kupotezwa?

Akamalizia kwa kuwakumbusha kiapo cha mkristo "Nitaheshimu viongozi wangu wa dini katika yale wanayonionya na kunielekeza" Tafakari.
 
Hivi masheikh ubwabwa wao hawatoi matamko kama haya kwa nini lakini?
 
"Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa). Sehemu muhimu ya siasa ni majadilianao kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka. Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi..."

kwa maana hiyo ya siasa, na kama kila mtu ataelewa hivyo, hakuna ubaya kwa mtu yoyote kujihusisha na siasa. watawala wengi wa tanzania wanadhani siasa ni vyama tu, au wakuu wa serikali tu, la hasha!

or see Politics
 
Hivi masheikh ubwabwa wao hawatoi matamko kama haya kwa nini lakini?

Tusiwadhalilishe hawa masheikh,tutafute tatizo la hawa watu kuitwa masheikh. Nimekuwa nikifuatilia mambo ya islam na hilo ni jambo ambalo baadhi linalowakosanisha na BAKWATA. Tatizo ni watu bora,wenye uelewa kukataliwa kila wanapojitokeza ktk chaguzi za uongozi. Angalia ubora wa sheikh mkuu?
 
Hoja hapa ni kuwa dini ni yetu sisi wananchi,viongozi wa dini ni sehemu ya viongozi katika jamii yetu hivyo siasa na dini ni chanda na pete.
 
Kuweka usanii wa kuandaa maaskofu feki hakusaidii kujenga taifa imara.
 
Hoja hapa ni kuwa dini ni yetu sisi wananchi,viongozi wa dini ni sehemu ya viongozi katika jamii yetu hivyo siasa na dini ni chanda na pete.


Mpeni Kaisari vilivyo vyake KAISARI na Mpeni Mungu vilivyo vyake Mungu, Huwezi kuwatumikia mabwana wawili??????!!!!!!!!!!!!!!!!!! chagua kuwa moto au vuguvugu!!! kama bado hujanielewa baadaye utanielewa tu!
 

Mmmmmmmm!!
 
Kuweka usanii wa kuandaa maaskofu feki hakusaidii kujenga taifa imara.

Goodrich ulitaka iweje?nani anaweka maaskofu feki? unajua kazi ya uaskofu inatokea wapi? na hao maaskofu feki unaowasema wanamuongoza nani nataka majibu acha kukurupuka!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…