Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safi sana Askofu,hakika ww si mnafiki,Mungu ambariki Dr Bagoza,Bishop
acha ujinga wewe tamko linaendelea kusomwa makanisani Halafu unaleta ubishi WA kijinga hapa.kwa taarifa yako Katika Katika kabisa katoliki askofu WA jimbo au Hata paroko WA parokia anasikilizwa kuliko kardinali.maaskofu wanateuliwa na papa hivyo kardinali hana ubavu wa kuingilia majukumu yako ndiyo maana hana ubavu WA kuzuia tamko la maaskofu kusomwa makanisani anabaki kulalamika tu.
Askofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amepinga vikali kauli ya serikali kwamba maaskofu wamegawanyika kuhusu Kura ya Hapana kwenye Katiba Mpya.
Askofu Bagonza ambaye ni mjumbe wa CCT ameonya kauli ya Samwel Sitta kwamba Serikali haitarudi nyuma kuhusu katiba mpya.
Askofu Bagonza ambaye ana msimamo thabiti amesema wapo maaskofu wa mfukoni wanaoandaliwa na Serikali ambao wanatumika kujibu hoja mbalimbali za kanisa.
Akizungumzia Kauli ya Kadinali Pengo kupingana na maaskofu wenzake, Askofu Bagonza amesema huo ni msimamo binafsi wa Kadinali Pengo na siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesema msimamo wa Kanisa Katoliki nchini unatolewa na TEC ambalo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesisitiza kwamba pamoja na msimamo binafsi wa Kadinali Pengo lakini ameruhusu Tamko la Maaskofu kusomwa katika Makanisa yote ya Jimbo lake la DSM.
Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.
Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================
Chanzo: Mwananchi
daaaah huyo askofu noma sana bonge la kichwa
Hivi masheikh ubwabwa wao hawatoi matamko kama haya kwa nini lakini?
Hivi masheikh ubwabwa wao hawatoi matamko kama haya kwa nini lakini?
Hoja hapa ni kuwa dini ni yetu sisi wananchi,viongozi wa dini ni sehemu ya viongozi katika jamii yetu hivyo siasa na dini ni chanda na pete.Katika ibada ya pasaka iliyofanyika katika usharika wa Kayanga dayosisi ya Karagwe Baba Askofu Dr Benson Bagonza aliwatolea uvivu wavivu wa kufikiri kwa hoja zifuatazo:
1. Sisi makanisa tunapojenga shule mbona hatuambiwi tunaingilia kazi za serikali?
2. Tunapojenga miradi ya maji mbona hatuambiwi tunaingilia kazi za wizara ya maji?
3. Tupoombea mvua mbona hatuambiwi tunaingilia mamlaka ya hali ya hewa?
4. Tunaposifia serikali mbona hatulaumiwi, lakini tunapokosoa tunakaribia kupotezwa?
Msemaji wa kanisa katoliki tanzania ni rais wa tec sio cardinal pengo,serikali inajidanganya tu,muda mwalimu mzuri sana.
Hoja hapa ni kuwa dini ni yetu sisi wananchi,viongozi wa dini ni sehemu ya viongozi katika jamii yetu hivyo siasa na dini ni chanda na pete.
"Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa). Sehemu muhimu ya siasa ni majadilianao kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka. Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi..."
kwa maana hiyo ya siasa, na kama kila mtu ataelewa hivyo, hakuna ubaya kwa mtu yoyote kujihusisha na siasa. watawala wengi wa tanzania wanadhani siasa ni vyama tu, au wakuu wa serikali tu, la hasha!
or see Politics
Kuweka usanii wa kuandaa maaskofu feki hakusaidii kujenga taifa imara.
Acha kashfa dogo ,mbona husemi wachungaji wazinifu.
Hivi masheikh ubwabwa wao hawatoi matamko kama haya kwa nini lakini?
We we we we ni hiki ati weye watuleta rudi kwenye mada tajwa plz twende sawa!!!