KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

Wasalaam wanajukwaa! Kwanza kabisa naomba kuelewa nini maana ya neno UANAHARAKATI? Kwa uelewa wangu wa kati ni kwamba hili linaweza kusadifiwa na mazingira husika, kuna wanaharakati wa kiimani, kuna wanaharakati wa kisiasa,wanaharakati wa kiuchumi nk.

Hivi dhambi ya kiongozi wa dini kufanya uanaharakati katika mazingira yake iko wapi? Ukisoma vitabu vya manabii wote waliopita utakuta wote walikua wanaharakati kwa kazi zoa katika jamii.

Suala la katiba ni la kisiasa lakini linapozungumzwa na kiongozi wa dini katika mahali pakuabudia sio kosa! ndiyo kazi yake, kama waumini hawana elimu juu ya katiba nani awaelimishe?

Kati ya mwanaharakati wa kisiasa na wa kiimani ni yupi anaweza kuaminiwa na jamii zaidi?

Inashangaza sana kuona kiongozi mkubwa wa kisiasa anakashifu viongozi wa dini kuwaita wamegeuka kuw wanaharakati, hii ni kukosa uelewa kwa baadhi ya viongozi wetu.
 
Ahsante sana maaskofu Kwa kusimama imara pamoja na hila nyingi watawala wanazofanya.

Acha maaskofu waionyeshe ccm nguvu yao kwenye hii nchi.

Naomba Mungu ccm waendelee kuwa na kichwa ngumu mpaka maaskofu watangaze kutoshirikiana na ccm kabisa
 
Ben Saanane MwanaDiwani Baraza la Maaskofu ni taasisi yenye nguvu.Waraka uneshasambazwa na Pengo hana uwezo wa kuzuia[/QUOTE said:
mkuu kwa kumkumbusha tu ni kuwa Pengo aliaagiza waraka upelekwe kwenye parokia zote na sasa parokia inafanya kazi ya kuusambaza kwenye jumuiya na kila ibada ya jumuiya waamini wanapata wasaa wa kutafakari waraka wa kichungaji
 
Mtu mwenye akili timamu unashabikia Tanzania iongozwe toka kanisani ajabu hii kisa unataka chama chako kichukue dola, bila kujali yatakayo tokea mbele.
Unataka kuingia lkulu kwa njia haramu aibu
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

Ungalikua unajua Pengo ni nani katika hierachy za kanisa katoliki hata usingeropoka kama ufanyavyo humu.

Pengo ni kardinali ni askofu kama maaskofu wengine Tanzania.

Kiuongozi TEC ndiyo yenye mamlaka ya kiutawala......Msimamo wa kanisa unatolewa na TEC.

Sasa msimamo wa Pengo as individual sio msimamo wa kanisa.

Ukizoea Kuishi kwa UNAFIKI kama ulivyo wewe na Ma CCM wenzako mtapata shida sana kutambua lililo haki na lisilo haki
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

Kauli ya Maaskofu wa Mfukoni sijui Cardinal Pengo ameielewa maana yake?
 
Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.

Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================

Chanzo:
Mwananchi

Huyu askofu ni kilaza wa mwisho, analinganisha kanisa na CCM na UKAWA. Kama sio kilaza basi anathibitisha kauli ya Pengo na Kilaini kuwa baadhi ya hao maaskofu wanamaslahi ya kisiasa.
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target![/QUach

Mkuu ulimwelewa Kakobe alivyokwambia lakini?juu ya two babes?
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

huna hoja wewe...kwanini mnalazimisha katiba ya ccm ndio itawale nchi huku mkikataa maoni ya wananchi? kulikuwa na haja gani ya kukusanya maoni sasa? magamba mmebanwa vibaya sana...kama mchusi abanwavyo na mlango, wapuuzi wakubwa!

kama mlitarajia kupata cheap votes kutoka kwa waislamu, imekula kwenu...elewa kwamba hata waislamu wenyewe walishakushtukia kitambo kwa hiyo peremende kanyaboya mnayotaka kuwalambisha. mtajibeba fisi wakubwa!
 
Huyu askofu ni kilaza wa mwisho, analinganisha kanisa na CCM na UKAWA. Kama sio kilaza basi anathibitisha kauli ya Pengo na Kilaini kuwa baadhi ya hao maaskofu wanamaslahi ya kisiasa.

Kwani CCM siyo watu? Ni wanyama au?
 
Mtu mwenye akili timamu unashabikia Tanzania iongozwe toka kanisani ajabu hii kisa unataka chama chako kichukue dola, bila kujali yatakayo tokea mbele.
Unataka kuingia lkulu kwa njia haramu aibu

Hatutaki chama chochote kichukue dola, tunataka hii nafasi tuitumie vizuri. Ni nadra kupata nafasi kama hii ya kuandika katiba upya, kwa kuwa tumeipata tuitumie vizuri.

Asiwepo mtu wa kujiona ana hati miliki ya kuburuza watu anavyotaka, badala yake tuchukue muda wetu bila haraka. Tutafakari na kujiridhisha ndipo tuseme ndio

Tunatamani tuwe na maridhiano wote ili tupate kilicho cha wote, haya tu.

Wala hapigiwi debe mtu, wala hakibebwi chama!

Wananchi wapate muda wa kutosha, walielimishwe juu ya yale yaliyomo na wajue yanayoachwa na sababu za kuachwa.
 
Ok Ok Swali la msingi bado linabaki kuwa Msiamamo wa Kanisa Katolika unatolewa na Pengo au na TEC? hahahaa Mpwa fikirisha kichwa sometimes bhana
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!

kwanini serikali IWAAGIZE wananchi waipigie katiba kura ya NDIYO badala ya kuwaacha wafanye maamuzi kwa utashi wao? umepewa kichwa ukitumie kufikiri, sio kufugia nywele. tafakari!
 
kwanini serikali IWAAGIZE wananchi waipigie katiba kura ya NDIYO badala ya kuwaacha wafanye maamuzi kwa utashi wao? umepewa kichwa ukitumie kufikiri, sio kufugia nywele. tafakari!

Hakika huyo kijana kichwa chake ni cha kufugia nywele.
 
CCM ni chama cha siasa, hayo ya kuwaambia wachague nini kwenye masuala ya siasa ndio jukumu lao. Sasa hao maaskofu ni chma cha siasa?

Na serikali ni nani? Mbona serikali inasema Katiba ni nzuri na watu wapige kura ya Ndiyo?

Tumia kichwa chako kifikiri na siyo kufugia nywele!
 
Kardinali Pengo alisema hivi;

Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!
acha ujinga wewe tamko linaendelea kusomwa makanisani Halafu unaleta ubishi WA kijinga hapa.kwa taarifa yako Katika Katika kabisa katoliki askofu WA jimbo au Hata paroko WA parokia anasikilizwa kuliko kardinali.maaskofu wanateuliwa na papa hivyo kardinali hana ubavu wa kuingilia majukumu yako ndiyo maana hana ubavu WA kuzuia tamko la maaskofu kusomwa makanisani anabaki kulalamika tu.
 
CCM ni chama cha siasa, hayo ya kuwaambia wachague nini kwenye masuala ya siasa ndio jukumu lao. Sasa hao maaskofu ni chma cha siasa?
kwa hiyo serikali na maccm wanavyozungumzia mambo ya mahakama ya kadhi kwani yenyewe ni madhehebu ya dini?
 
Mimi nitaamini Waraka wa Baraza la Maulamaa na sio Bakwata ya ccm
 
Back
Top Bottom