MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Wasalaam wanajukwaa! Kwanza kabisa naomba kuelewa nini maana ya neno UANAHARAKATI? Kwa uelewa wangu wa kati ni kwamba hili linaweza kusadifiwa na mazingira husika, kuna wanaharakati wa kiimani, kuna wanaharakati wa kisiasa,wanaharakati wa kiuchumi nk.
Hivi dhambi ya kiongozi wa dini kufanya uanaharakati katika mazingira yake iko wapi? Ukisoma vitabu vya manabii wote waliopita utakuta wote walikua wanaharakati kwa kazi zoa katika jamii.
Suala la katiba ni la kisiasa lakini linapozungumzwa na kiongozi wa dini katika mahali pakuabudia sio kosa! ndiyo kazi yake, kama waumini hawana elimu juu ya katiba nani awaelimishe?
Kati ya mwanaharakati wa kisiasa na wa kiimani ni yupi anaweza kuaminiwa na jamii zaidi?
Inashangaza sana kuona kiongozi mkubwa wa kisiasa anakashifu viongozi wa dini kuwaita wamegeuka kuw wanaharakati, hii ni kukosa uelewa kwa baadhi ya viongozi wetu.