KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

KKKT : Maaskofu hatujagawanyika kuhusu Katiba

Kumbe nabishana na mtu asiyejitambua...

Utabaki kupiga makitaimu ta hapa lakini Tamko la Maaskofu limeshatolewa na sasa kila mwanajumuiya analo.

Kila mikutano ya wanajumuiya sasa msisitizo ni kutii mamlaka ya Kanisa ya Kura ya Hapana kwa Katiba Haramu ya Chenge na Mafisadi.

Matamko ya jumuia hayakuanza leo, kama umesahau waraka wao mwaka 2010 uliwaamuru watu wasiichague CCM na Kikwete lakini leo unajua rais wa JMT ni nani. Hao watatoa kila tamko ila mwenye mamlaka ya mwisho ya kuamua ni mwananchi. Kama nyie wafuasi wao mnapenda kuamuliwa huo nao ni uhuru wenu. Alichokisema Pengo na Kilaini ni kuwakumbusha hao vilaza kuwa waumini wa dini za kikristo wana akili zao timamu na wanajua wanachokitaka hivyo wataamua wanataka nini.
 
11082500_10153156133462359_5931312413025622367_n.jpg

Na wote tuseme Amen na Hapana kwa Katiba Pendekezwa - Hongera kwa Maaskofu waliliona hili.
 
Kama serikali inawashawishi wananchi wapige kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa kwa kuwa inaamini kuwa ndiyo wazo sahihi ni kwa nini jumuia ya maskofu iwe mwiko kuwashawishi waamini wao wapige kura ya hapana ikiwa na wao wanaamini kuwa ndiyo wazo sahihi? Kama kwa kufanya hivyo serikali inaamini kuwa haiwaamulii wananchi juu ya nini wana kitaka kwanini iwe maaskofu waonekane wanawaamulia wananchi kitu wanachokitaka. Ni kwa nini serikali iwe na haki ya kuwaamulia wananchi ila kundi lingine la viongozi iwe mwiko kufanya jambo lielile ambalo viongozi wenzao wa kisiasa wanalifanya? Ni nani kawaloga viongozi wa kisiasa kudhani kuwa wana haki zaidi ya makundi mengine yote yaliyopo nchini? Tena hata mke wa Raisi tumemsikia akiwashawishi wananchi wapige kura ya ndiyo kwa katiba inayopendekezwa, huyu anayo haki ya kuwaelekeza wananchi nini cha kufanya ila viongozi wa kidini hawana haki, nani kawapa haki viongozi wa kisiasa kufikiri kwa niaba ya watu wengine?
Askofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amepinga vikali kauli ya serikali kwamba maaskofu wamegawanyika kuhusu Kura ya Hapana kwenye Katiba Mpya.

Askofu Bagonza ambaye ni mjumbe wa CCT ameonya kauli ya Samwel Sitta kwamba Serikali haitarudi nyuma kuhusu katiba mpya.

Askofu Bagonza ambaye ana msimamo thabiti amesema wapo maaskofu wa mfukoni wanaoandaliwa na Serikali ambao wanatumika kujibu hoja mbalimbali za kanisa.

Akizungumzia Kauli ya Kadinali Pengo kupingana na maaskofu wenzake, Askofu Bagonza amesema huo ni msimamo binafsi wa Kadinali Pengo na siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Askofu Bagonza amesema msimamo wa Kanisa Katoliki nchini unatolewa na TEC ambalo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini.

Askofu Bagonza amesisitiza kwamba pamoja na msimamo binafsi wa Kadinali Pengo lakini ameruhusu Tamko la Maaskofu kusomwa katika Makanisa yote ya Jimbo lake la DSM.

Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.

Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================

Chanzo:
Mwananchi
 
Hawa UKAWA nao kumbe wapuuzi sana, yaani wameambia watu wasusie.. Hivi hapo si ni kuwapa Wahuni ushindi??

Haraka sana UKAWA hamasisheni watu wakapige kura ya HAPANA iwapo serikali itang'ang'ania kura ipigwe.
 
Nimemsikia JK akiwaambia ma-DC wateule pale Dodoma eti waende kusimamia kura ya maoni itakayofanyika April 30. Unajua mimi nashangaa hivi huyo rais na waziri wake wa sheria hawajui ukweli wa mchakato au wameamua kutengana na akili zao? Ukweli ni kwamba hakuna kura ya maoni kwa sababu kuu mbili. Kwanza taratibu na sheria kwa mujibu wa Sheria ya kura ya maoni haujafuatwa. Hilo ni suala la kisheria nk JK na migiro kama wanaamini katika utawala wa sheria waache mara moja kudanganya Watanznia eti kuna kura ya maoni. Pili BVR ni mshipa kama sio tezi dume. Hilo zoezi hiliwezi kwisha kabla ya mwezi juni. Hata hivyo nahisi hila moja ambayo Watanzania wanaandaliwa kisaikologia ili kwa kuwaambia kura ya maoni ni vilevile ilivyopangwa na jk. Watazuka na hoja fulani ambayo watalazimisha watu wapige kura ya maoni bila daftari la wapiga kura hata ikibidi kunyosha vidole na kupitisha katiba lao bila muafaka.
 
Mimi sijui nani kasema nini. Ninachojua ni kura kwa katiba mpya ni HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA ..........................................................................................HAPANA!!!!! TUUNGANE
 
Yaani serikali ya JK kama beki ya man city...mabeki watatu wanapigwa chenga na mtu mmoja yaani ni full kupagawa..
 
Nimemsikia JK akiwaambia ma-DC wateule pale Dodoma eti waende kusimamia kura ya maoni itakayofanyika April 30. Unajua mimi nashangaa hivi huyo rais na waziri wake wa sheria hawajui ukweli wa mchakato au wameamua kutengana na akili zao? Ukweli ni kwamba hakuna kura ya maoni kwa sababu kuu mbili. Kwanza taratibu na sheria kwa mujibu wa Sheria ya kura ya maoni haujafuatwa. Hilo ni suala la kisheria nk JK na migiro kama wanaamini katika utawala wa sheria waache mara moja kudanganya Watanznia eti kuna kura ya maoni. Pili BVR ni mshipa kama sio tezi dume. Hilo zoezi hiliwezi kwisha kabla ya mwezi juni. Hata hivyo nahisi hila moja ambayo Watanzania wanaandaliwa kisaikologia ili kwa kuwaambia kura ya maoni ni vilevile ilivyopangwa na jk. Watazuka na hoja fulani ambayo watalazimisha watu wapige kura ya maoni bila daftari la wapiga kura hata ikibidi kunyosha vidole na kupitisha katiba lao bila muafaka.

Acha kupoteza muda wako kumsikiliza huyo..aliwadanganya kigoma itakuwa dubai lakini mpaka leo ni afadhali ya kishumundu kuliko kigoma dubai
 
Matamko ya jumuia hayakuanza leo, kama umesahau waraka wao mwaka 2010 uliwaamuru watu wasiichague CCM na Kikwete lakini leo unajua rais wa JMT ni nani. Hao watatoa kila tamko ila mwenye mamlaka ya mwisho ya kuamua ni mwananchi. Kama nyie wafuasi wao mnapenda kuamuliwa huo nao ni uhuru wenu. Alichokisema Pengo na Kilaini ni kuwakumbusha hao vilaza kuwa waumini wa dini za kikristo wana akili zao timamu na wanajua wanachokitaka hivyo wataamua wanataka nini.
Ndio lakini matokeo yake ni nini?
 
asante sana askofu wangu.....

Naomba askofu wangu wa dayosisi ya kaskazini na wewe uuunge mkono kura ya hapana.....hii katiba sio chaguo la wananchi.....

mtaishia kusema hivo hivo lakini hii inapita, elimihseni watu waisome na sio kuwaambia eti wapige kura ya hapana, hapo mnachemka!!
 
acha kupoteza muda wako kumsikiliza huyo..aliwadanganya kigoma itakuwa dubai lakini mpaka leo ni afadhali ya kishumundu kuliko kigoma dubai

huna hoja tushakuzoea na ajenda zako zisizo na mantiki, soma katiba kuwa mzalendo waelimishe wenzio uzuri wa katiba inayopendekezwa!!
 
Ni kweli ili kupata kitu kizuri lazima kichwa kisiwe cha nywele tubali kifanye kazi yake na ikiwezekana kazi ya ziada. Tukidgahitambua na kutambua mchakato uliotumika kupata katiba tutapata jibu wakati wa kura ya maoni
 
Msemaji wa kanisa katoliki tanzania ni rais wa tec sio cardinal pengo,serikali inajidanganya tu,muda mwalimu mzuri sana.
Hivi aliyetakiwa kuwawajibisha akina Kilaini na Nzigilwa kwa zile mil 40 walizopata kila mmoja kwenye mgao wa Escrow ni nani? Isije kuwa vumbi lake limemuathiri maana inawezekana wengine walichukuliwa kwa niaba
 
Pengo ana mamlaka kwa jimbo lake tu na si majimbo mengine. Msemaji wa TEC ni rais wake. Kura ni hapana
DINI ndiyo iliyozaa siasa, hapa nchini na kwa kutumia mwanya wa UFINYU wetu wa KUFIKIRI tunaona siasa ndiyo iliyozaa DINI! Pengo, Kilaini na washirika wao tunapaswa kuwaombea kwani sasa si watumishi wa Mungu tena ila wanawtumkia watawala wa nchi.
 
and the vice versa is true to you adoring fake priests whom you used to adore them as if they are you Gods!!
 
mbona watz mna papara hivyo? Hiyo kura yenyewe haiwezekani kupigwa hiyo tarehe 30/04/2015. Kama imechua takriban mwezi mmoja kuandisha watu ktka daftari la wapiga kura katika mkoa mmoja,

je mikoa iliobaki itachukua muda gani kwa utaratibu huu? Jiulize.! Kwa hiyo kimsingi kama utaratibu wa kuandikisha wananchi kwenye daftari la wapiga kura utaendelea kufanyika kwa staili ya sasa , basi tusahau kupiga kura 30/04/2015 labda wapange tarehe nyingine!

kura ya maoni iko palepale, we wapi wewe usiyejua hata taarifa kwenye vyombo vya habari? Taarifa hiyo ulosema kaisema nani? Lini? Na wapi? Acha kupotosha watanzania kwa vitu vyako binafsi bhana.
 
Back
Top Bottom