KKKT mmekubali kukumbatia Nyoka, acha awang'ate, Shetani hana rafiki

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
9,205
Reaction score
22,219
Alichokifanya Makonda hapo kanisa la KKKT ni utovu mkubwa sana wa nidhamu. ndo maana watu wote walikuwa wanamshangaa tu akiendelea kubwabwaja utopolo.

Huwezi kupewa microphone 🎀 kanisani halafu uanze kuwasema vibaya maaskofu wanaokosoa serikali na kudhinda mtandaoni.

Kanisa na maaskofu wana wajibu wao kiroho lakini kama raia kutoa maoni yao kwa nchi kama wazalendo wengine. Makonda hana mamlaka ya kuwaelekeza nini cha kufanya wana miongozo yao.

Tunamjua.Bangonza . kitima Gwajima na wengine ni wakosoaji wakubwa sana wa serikali.

Kwa kuwa KKKT wamekubali kukubatia Nyoka siku moja atawatoa uhai . Nyoka hanaga urafiki na mtu. TEC waliona mbali sana.
 
this is the most nonsense article of the day gentleman πŸ’
 
Kama kuna makosa makubwa hilo kanisa au huyo mtumishi kufanya basi ni kumpa MIC huyo mwanasiasa kutoa neno, mahali pa kuabudia ni sehemu TAKATIFU sana. Hakupaswi kuchanganywa na mambo kama hayo.

Inafikirisha na kusikitisha kuona Kanisa/Watumishi wamefikia hatua ya kuidharau madhabahu kiasi hiko.
 
ni wapi huko tapeli DAB alipewa airtime
 
Huwezi kupewa microphone 🎀 kanisani halafu uanze kuwasema vibaya maaskofu wanaokosoa serikali na kudhinda mtandaoni.

Makonda huyo huyo siku moja kabla ya hiyo hadhara ya KKKT alikuwa analalama kwamba katiba inaruhusu mtu kutoa maoni...
Yeye katoa maoni yake kuhusu jezi na kajitetea kwamba amepata mamlaka hiyo toka kwenye katiba ya JMT ya uhuru wa maoni...

Lakini serikali na viongozi wake wanapokosolewa na watu wa makanisa, Bwana Makonda anaona huko ni kuvuka mipaka...

Hii ni ajabu!
 
Tatizo linaanzia KKKT ni kanisa la wachagaπŸ₯ΉπŸ₯Ήwachaga wepesi sana kununulika wanapoona Kuna sehemu ya Hela na itakuwa Konda Boy alitoa sadaka ya pesa ndefu si ni mbunge wao wa huko Arusha
 



View: https://www.youtube.com/watch?v=D7wVY4Ltduw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…