KKKT waunga mkono uwekezaji Bandarini, TEC nao wataunga tu

KKKT waunga mkono uwekezaji Bandarini, TEC nao wataunga tu

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha.

=========
Nukuu ya alichozungumza Askofu Shoo
Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono Uwekezaji, hatupingi Uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha wakati wa maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa hilo.

Screenshot_20230821_134948_WhatsApp.jpg

VIDEO:
View attachment 2724093
 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT jijini Arusha ameeleza kuwa viongozi wa dini wakiwemo KKKT, TEC, BAKWATA, CCT na wengineo walikutana na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwanzo na kuzungumza kwa mapana juu ya suala la uwekezaji wa kampuni ya DP World katika bandari ya Dar Es Salaam.

Katika kikao hicho, viongozi wa dini waliwasilisha maoni yao ikiwemo matatizo wanayoyaona na Serikali imeahidi kuyafanyia kazi.
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha.
Kasema lakini.......!!! Acha upotoshaji tupo live hapa.

Na amesema Viongozi wa dini tukikemea acheni kusema tunachanganya dini na siasa.

Lofa wewe
 
Japo hajatamka bayana kama ni uwekezaji wa Bandari au laa ila askofu Shoo amesema wanaunga mkono Uwekezaji kwa kuwa wanatambua ndio njia kubwa ambayo mh.Rais anaitumika kukuza maendelea ya Watanzania.

View: https://twitter.com/eastafricatv/status/1693577838094323980?t=B5kjt2aYv3TJFWI_j8JtwA&s=19

My Take

Kwa kuwa Viongozi wa dini kuu Kwa umoja wao walienda kumuona mh.Rais na wakatoa maoni Yao ,hii ya TEC inatoka wapi? Je Kuna mahala mh.Rais amekataa maoni ya watu?

Mods huu sio Uzi wa Kidini.
 
Kamchana live bila kupepsa macho.kasema kabisa kama hawatazingati ushauri waliokubaliana basi wakianza mashambulizi wasiaambie kuwa wasichanganye dini na siasa.kingine kamwambia inakuwaje makaa ya mawe kila siku yanauzwa na faida hatuoni?kwa nini tusiyachakate wenyewe.Kazi kwenu machawa wa mama.
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa msimamo wa kuunga mkono Uwekezaji wa Bandari.

Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu FREDRICK SHOO ametoa msimamo huo leo Agosti 21, 2023 Mkoani Arusha.
Issue ya Dp world amesema wazingatie ushauri wao. Hajasema wanaunga mkono uwekezaji wa Bandari huu ni uongo na naona same message mnaizungusha mitandaoni.

BTW hili pia limechangiwa na Dr Shoo kushindwa kunyoosha maelezo. Obvious hotuba ya Shoo leo itatumika vyema mitandao yote [emoji1787]
 
Back
Top Bottom