The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
"Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe"
"Ninatambua kuwa ulipokea kijiti katika mazingira magumu sana, lakini pia pamoja na mazingira yale wewe ukaanza historia mpya ya nchi yetu ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais, kuna wengi hawakuamini, hawakutaki na mpaka leo wamebaki na jinamizi la namna hii, huu ulikuwa ni mpango wa Mungu"
"Najua katika jambo hilo linaelekea mahali tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi, nashukuru Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi, umekaa kimya" - Askofu Dk Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Miaka60YaKKKT