Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Frederick Shoo, ametangaza kusitisha matamasha yote yanayoambatana na maadhimisho ya Pasaka, lengo likiwa ni kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.
"Panahitajika elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa COVID-19, niwaombe Watanzania kuacha kufanya mizaha. Tuache tabia iliyoibuka kwa baadhi ya watu kushangilia, pale viongozi wa kitaifa wanapopata ugonjwa huo"
Pia ametoa angalizo kwa wanaotengeneza na kuuza dawa za asili kutofanya kwa maslahi binafsi tu.
"Mnaotoa dawa za asili, msitumie kama fursa y kutengeneza biashara kwa kuwa tu, watu wanataka kupona na kujikinga"
"Kama Watanzania wataacha mizaha na kushirikiana na wataalamu wa afya pamoja na kumuomba Mungu, ninaamini, wimbo la ugonjwa wa COVID-19 litapita kwa uwezo wake"
"Katika janga la Corona hatari sio kwa wale waliokwishafariki bali ni sisi hapa tunaopumua na kukohoa ndio wenye hatari ya kuambukizana. Nawaombeni sana, isiwe aibu wala isionekane ni kosa la imani kuvaa barakoa"