KERO KKPESA: Benki Kuu ifuatilie hii kampuni ya Mkopo

KERO KKPESA: Benki Kuu ifuatilie hii kampuni ya Mkopo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nilishawahi sema wabongo wengi hatuko tayari kufuata sheria wala makubaliano kwenye mikataba. Tuna chembechembe za utapeli na dhuluma. Kama ulikopeshwa pesa na ukakubali kurejesha na riba kwanini usirejeshe kama ulivyokubali?
Ndio Maana Watz tuko hivi Tulivyo, basi kama unadharura omba msamaha na uahidi ni lini utalipa lakini jitu linakaza fuvu likitaka mutapeli
 
Hao jamaa ni matapeli, lakin wanabadilisha kibao wanakuita wewe ndo una mpango wa kuwatapeli.

 
Hao jamaa ni matapeli, lakin wanabadilisha kibao wanakuita wewe ndo una mpango wa kuwatapeli.

Hahaha
 
Hao jamaa ni matapeli, lakin wanabadilisha kibao wanakuita wewe ndo una mpango wa kuwatapeli.

Nyie ndio mnakatwa Vichwa mnakula hela za watu na bado mnatamba
 
Yaani wewe mleta mada una bahati sana maana hawa jamaa wanakupiga tu mikwara. Nimeshuhudia wafanyakazi wezangu watatu wametukanwa matusi ambayo hayasemeki na yakasambazwa kwenye group la ofisi na bado pia kwenye group zao mbali mbali za whatssap zikiwapo za familia. Aisee ukiwa na shida hata ya namna gani achana kabisa na hao wakopeshaji uchwara utaadhirika jamaa hawajali kwenye group za familia huko kuna watu wa karibu kabisa kifamilia wao wanaruka na wewe kiulaloulalo huko huko.
 
ukiwaogopa wanakupa hofu ya kijinga sana. mimi baada ya kunipa tu hela nikafuta premission zote za app yao kisha nikaifutilia mbali..
 

Attachments

  • Screenshot_20260523-200512.jpg
    Screenshot_20260523-200512.jpg
    124.7 KB · Views: 18
Kuna application hii ya kutoa mikopo mitandaoni inaitwa KKPESA naombeni muifuatilie kwa ukaribu sana.

1. Riba zao ni kubwa na inatakiwa mkopo ulipwe kwa muda mfupi sana siku 7.

2. Siku ya 6 kabla ya kufika siku ya rejesho wanakushurutisha ulipe deni kwa nguvu kwa kutoa maneno ya kejeli na sms za vitisho.

3. Wanatafuta watu/contact list yako bila ridhaa yako na siku ambayo hujapitisha rejesho. Naombeni mtusaidie ni scam application inatunyonya Watanzania na kutokana na ugumu wa maisha unajikuta umeingia kwenye mfumo wa kuchukua fedha katika application hiyo.

Kwa elimu yangu ndogo najua haifuati sheria za mikopo katika ukubwa wa riba. Watu wanateketea na kutapeliwa hela zao kutokana na hii application.

Naomba kuwasilisha🙏🏿🙏🏿

View attachment 3593022View attachment 3593023View attachment 3593024View attachment 3593025
Una bahati sana hata kule kufanikisha kuwakopa!

Hao ni matapeli wa kimtandao ambao Serikali inawalea, ama ni miradi ya viongozi wa Serikali kunyonya wananchi, hakuna lugha nyingine ya kulisemea jambo hili.

Kwanza wanadanganya kiasi cha mkopo kuwa ni kikubwa kumbe uongo tu.

Nilichogundua ni kwamba wananufaika zaidi kwa kuuza app hizo za mkopo.

Maana unapoapply mkopo utaambiwa haujafanikiwa rudia tena na app uliyodownload haifanyikazi tena mpaka udounload upya.

Mwishoni unakuja kupewa mkopo wa fedha kidogo sana, kiasi ambacho wala hujaomba.

Usiwalipe wakutangaze watakavyo, maana kila mtu ashawajua, ni washenzy sana.
 
Hizo huenda ni kampuni za waziri mkuu au jimama, unadhani watazichunguzaje?
 
Hao jamaa ni matapeli, lakin wanabadilisha kibao wanakuita wewe ndo una mpango wa kuwatapeli.

Wewe ni mpuuzi na ni hatari kwa usalama wako. Acha hii tabia.
 
Back
Top Bottom