Klabu Bingwa Barani Afrika: Waarabu Esperance na Wydad Casablanca watinga fainali

Mkuu...ukweli ni kwamba vilabu vyetu havina pesa ya kusajili cream...na mbaya zaidi hatuna mfumo mzuri wa kuzalisha hizo cream....lakini hata hizo chache tunazokua nazo zinachukuliwa na timu zenye uwezo.
Samatta na Patrick Ochang walinunuliwa na TP Mazembe lakini Simba haina uwezo wa kumnunua mchezaji tegemeo wa TP Mazembe....Mfano juzi tu Ameuzwa Makusu wa As Vita huko Morocco kwa 1.3 bilion ya Tanzania na mshahara wake kwa mwezi ni takriban 8.5 Milion ya Tanzania kwa mwezi... naweza kusema vilabu vyetu havina uwezo wa kufanya hivi...ndo mana hata wachezaji wakigeni kwetu wengi hawechezi timu zao za taifa wanakuja kuhustle tu huku.
 
Tp mazembe hawakua kwenye kiwango cha kufika final

Nawasikitikia mamelod sundown, maana uwezo walikua nao.
Uliangalia mpira au ndo unasoma comment tu huku hadi useme mazembe hawakua na kiwango cha kufika final.Kumbuka wamecheza na esperance timu ambayo haijafungwa hata mchezo mmoja toka mashindano yameanza.
 
Tusubiri msimu ujao, lakini tunakosea wapi?
Siamini kama hili swali bado hujalipatia majibu hadi sasa, POLITICS NDUGU, kila kitu tunaleta siasa, ngoja nikupe shuhuda mbili ya kwanza ilitokea Zanzibar kuna mtu alinyimwa uongozi chama cha soka huko visiwani kisa ana kadi ya CUF, pili kuna mbunge wa upinzani mikoa ya kusini alienda kuisaidia timu pesa viongozi wa timu wakamkimbia sasa jiulize viongozi wa timu kumkimbia mbunge anaetaka kuwasaidia walikuwa wanaogopa nini?
 
Wale vyuraa walio kua wakishagilia mzembe sura zenu mmezificha wapi. ?
 
Tukijifunza kwamba siasa si uadui, na maendeleo hayana chama labda itaeleweka.
 
Du,
 
Nina uhakika kama simba angecheza fainali na mwarabu yoyote kati ya hao tajwa hapo juu. Simba angekuwa bingwa
 
Mwarabu wa kwanza kafa 3-0 na wa pili kafa 1'0 hapa mkuu. Kwa simba mwarabu mwepesi kama kimsukuma mlevi
Mmeshindwa mazembe ndio mumuweze mwarabu? Au unamtaka magoli matano yajirudie tena?
 
Mwarabu wa kwanza kafa 3-0 na wa pili kafa 1'0 hapa mkuu. Kwa simba mwarabu mwepesi kama kimsukuma mlevi
kwanzia robo fainali ni game mbili tu moja ugenini na moja nyumbani. Hadi fainali ipo hivyo hivyo, sasa tupe rekodi ya Simba ikiwa ugenini. kafungwa tano na Al Ahyl ugenini . Je huyu bingwa mtetezi mngewezaje kumtoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…