Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Baada ya kupokea kichapo kizito cha goli 4-1 kutoka kwa PSG katika Dimba la Camp Nou, Barcelona leo inatupa tena karata yake ya pili kuvaana na PSG ikiwa nyumbani katika uwanja wa Parc des Princes.
Huu ni mchezo wa marudiano wa hatua ya mtoano ambapo katika mchezo wa kwanza Kylian Mbappè aling'ara baada kuweka kambani goli tatu (hat trick).
Ili kuweza kuendelea kwenye hatua inayofuata Barcelona inahitaji kufunga goli 4-0 au zaidi.
Barcelona imekuwa katika kiwango kizuri na haijapoteza mchezo tangu Februari 16 ilipopoteza mbele ya PSG, huku miamba hiyo ya Ufaransa ikishinda michezo mitatu mfululizo.
Kwingineko takwimu zinaonesha kuwa Liverpool haijawahi kutolewa kwenye mashindano ya Ulaya kwenye hatua ya mtoano baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa ugenini.
Baada ya kutoa kichapo cha gi 2-0 kwa RB Leipzig katika uwanja wake wa nyumbani, Liverpool imekuwa na wakati mgumu baada ya kupoteza michezo mitatu na kushinda mmoja tu dhidi ya Sheffield United.