Klabu kubwa kama Simba SC, hii ni fedheha

Klabu kubwa kama Simba SC, hii ni fedheha

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kuna baadhi ya vitu vinaweza kukufanya ujifikiria mara mbili kama ulifanya chaguo sahihi kuwa shabiki wa Simba CS. Kuna upuuzi fulani ulifanywa na Utopolo FC kwa kumbeba mhabeshi alipokuwa akiwasili uwanjani Airport akitokea Congo. Ile picha iliwachoresha sana. Kwa mtu mshamba ambaye haijui vizuri bongo anaweza akasema kweli watanzania wanapenda sana mpira, ila kwa sisi tulio ndani tumelichukulia lile tukio kama kumbusho ya enzi za utumwa ambapo tulikuwa tukiwabeba wazungu kwa namna ile.

Hapo jana msemaji wa wetu wa Klabu akiwa mbele wa watanzania takribani 60,000 elfu alimpiga busu mwanaume mwenzake, tena busu la ugotini. kitu ambacho kilichochea baadhi ya wanachama kujiona kama tumefedheheshwa, kukaa kote bongo Okwi hajawahi kupigwa mabusu na uwezo wake aliokuwa nao. leo hii unampiga mabusu Mzambia tena live kabisa. Hizi mambo za kupiga mabusu wanaume wenzako zinaenda kinyume kabisa na tamaduni za kitanzania.

Tumefanya ujinga wa zaidi ya ule wa Yanga wa kumbeba mhabeshi kwa sababu ameenda kuchukua wachezaji Vita Club.

Capture1.PNG
 
Huu ulioandika ndio Utopolo unless umeanza ushabiki juzi ndio utakua unaliona hili tukio kwa mara ya kwanza ila katika soka hii imetokea mara nyingi sana.
 
Wivu mbaya sana. Ulitaka apigwe busu la makalioni kama wewe?
 
Mimi ni shabiki nguli wa Young Africans Sc lakini kwa tukio lile la jana hatupaswi kushangaa wala kuhoji sababu ni kawaida sana kwenye mchezo wa Soccer.
 
Mashabiki wa Utopolo bado wanaishi kwenye zama za kizamani.
Haya mambo ya another level hawawezi kuelewa .
 
Klabu za ovyo ovyo

Wale wengine wanambeba mtu Kama Mwinyi

Huku kwengine mtu anabusu mguu Kama mjinga fulani

Mara yule analeta siasa kwenye mpira

Kuanzia mfadhilj mpaka anaowafadhili wote akili Yao moja

Shwain
 
Back
Top Bottom