Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

CAF yaifanyia Ubaya Ubwela Simba SC

==

Timu ya Simba Sports Club imeamriwa kucheza mchezo mmoja bila mashabiki na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufuatia vurugu zilizotokea Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mechi dhidi ya CS Sfaxien.

Adhabu hiyo itaathiri mchezo wao wa nyumbani dhidi ya CS Constantine, utakaochezwa Jumapili, Januari 19.

Soma: CAF yazuia Mashabiki Sfaxien Kwenye Mechi dhidi ya Simba
1736862559742.png
Simba SC pia imetoza faini ya dollars Elfu 40 (TSh. Milioni 100,037,200) na imetakiwa zilipwe ndani ya siku 60.

Taarifa rasmi ya Klabu ya Simba
1736864550095.png
 
Hii ni habari njema kwa utopolo..ndo maana wamelipa mamilioni yao chap waliyokua wanadaiwa ya usajili ili waje wacheke...nasikia wamelipa jana...labda walishajua kuna adhabu ya mnyama inakuja... 😆
Kwaiyo yanga kulipa mamilioni kunahusianaje na ujinga wenu wa kuvunja viti? Yanga ndio waliwaambia mvunje viti?
 
Back
Top Bottom