Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Jambo la maana ni kwamba tayari simba imeshafuzu.
Hivyo Simba ikishinda mchezo wa Jumapili, itaongoza kundi lake na kufanya mchezo wa kwanza wa robo fainali utachezwa ugenini. (Huko hakuna athari yoyote kwa mashabiki wake)

CAF wamefanikiwa kuharibu sherehe tu ya tarehe 19 January
 
Klabu ya Simba itacheza mechi zake mbili za CAF bila ya mashabiki kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo dhidi ya Cx Sfaxien. Aidha club ya 5imba imetozwa faini ya 40,000 USD ambayo inatakiwa kulipwa kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
 
Hapa ni lazima niusifu uwekrzaji wa yanga nje na ndani ya uwanja.
Yanga ina watu wana roho mbaya huwezi kuamini hawakupenda na hawakuwa na furaha mashabiki wa Simba kupewa tuzo ya mashabiki bora.
Walifanikiwa kupandikiza watu walioonekana kama mashabiki wa Simba na wakang'oa viti ili kuichafua brand ya Simba.
Kuna mashabiki wanavaa jezi za Simba lakini ukweli wanaipenda yanga na kutwa kuisema vibaya Simba.
Simba tujifunze kuzuia madhara ya watu kama hawa mapema
 
Ni mashabiki wa mwiko nyuma ndo walivunnja....unadhani pale walikuwepo simba peke yao..kina Mchome chura ndo walivunja
Kwaiyo wamefungiwa kina mchome? Mchome ni shabiki wa yanga? Ata kama alivunja mchome Ina maana yeye ndie alivunja viti 250 ndani ya dakika chache? Ebu acheni ujinga wenu basi!
 
Klabu ya Simba itacheza mechi zake mbili za CAF bila ya mashabiki kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo dhidi ya Cx Sfaxien. Aidha club ya 5imba imetozwa faini ya 40,000 USD ambayo inatakiwa kulipwa kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
Ndo watajua hawajui.
 
JAMANI HATUNA HASARA TULISHAFUZUU...NA IKAWE FUNDISHO KWA WAARABU WENGINE UCHWARA...YANI MUANZISHE FUJO MUANGALIWE TENA MKO KWA WATU TENA NA VITI MTOE....PUMBAVUUU
 
Safi sana, uhuni ni wa kukomesha kwenye michezo.
Ni kweli Mimi ni Simba ila walichofanya wenzetu hakikua Sawa.

Mungu atuepushie mbali team yetu ilikua ikisifika kwa mashabiki wazuri na heshima.

Ni funzo pia.
 
Wakuu

CAF yaifanyia Ubaya Ubwela Simba SC

==

Timu ya Simba Sports Club imefungiwa michezo miwili na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya vurugu za Benjamin Mkapa mchezo dhidi ya CS Sfaxien. Mchezo wao dhidi ya CS Constantine Jumapili Januari 19 na mchezo mmoja wa robo fainali kucheza bila mashabiki wao.

Soma: CAF yazuia Mashabiki Sfaxien Kwenye Mechi dhidi ya Simba
Simba SC pia imetoza faini ya dollars Elfu 40 (TSh. Milioni 101,082,186) na imetakiwa zilipwe ndani ya siku 60.

Simba SC imepanga kutoa taarifa rasmi kwa mashabiki wao muda mchache ujao.
Wanathiiiimba.... 5imba Thiiimbaaaa 5imba Guvu Moya..
 
Kwaiyo wamefungiwa kina mchome? Mchome ni shabiki wa yanga? Ata kama alivunja mchome Ina maana yeye ndie alivunja viti 250 ndani ya dakika chache? Ebu acheni ujinga wenu basi!
Ww mchone ni lishabiki lenu bwabwa lile...
Nimelitolea tuu mfano....
Alieanza kutoa viti ni nani?? Ww ulikuwepo uwanjani? Ripoti ya polisi ilisemaje..
na ndo tushawabamiza na robo tumeenda...
 
Jambo la maana ni kwamba tayari simba imeshafuzu.
Hivyo Simba ikishinda mchezo wa Jumapili, itaongoza kundi lake na kufanya mchezo wa kwanza wa robo fainali utachezwa ugenini. (Huko hakuna athari yoyote kwa mashabiki wake)

CAF wamefanikiwa kuharibu sherehe tu ya tarehe 19 January
Bila mashabiki hamuwezi kufuzu nusu fainall 😀
 
Hii habari siiamini mpaka nitakapoona taarifa rasmi. Mimi ni mtu ambaye nikisoma kitu chenye ukakasi mtandaoni sikiamini mpaka nitafute vyanzo vitatu vya uhakika vya kusapoti taarifa hiyo. Mpaka sasa sijaona chanzo chochote kilichoripoti hili.
 
JAMANI HATUNA HASARA TULISHAFUZUU...NA IKAWE FUNDISHO KWA WAARABU WENGINE UCHWARA...YANI MUANZISHE FUJO MUANGALIWE TENA MKO KWA WATU TENA NA VITI MTOE....PUMBAVUUU
Hasara kubwa! Yaani mcheze robo fainali bila mashabiki mtarajie kufuzu nusu??
 
Ww mchone ni lishabiki lenu bwabwa lile...
Nimelitolea tuu mfano....
Alieanza kutoa viti ni nani?? Ww ulikuwepo uwanjani? Ripoti ya polisi ilisemaje..
na ndo tushawabamiza na robo tumeenda...
Kwaiyo ripoti ya polisi ilisema mchome ndio kavunja viti? Mashabiki wenu awajielewi kwani ni mara ya kwanza kuvunja viti? Tulieni dawa iwaingie na iyo ni rekodi nyingine ya ovyo mmeiweka baada ya Ile ya kuchoma moto uwanja kule afrika kusini Tena kwenye michuano iyo iyo ya wakina mama sijui uwa mna matatizo Gani nyie watu!
 
Back
Top Bottom