Klabu ya Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji Moses Phiri

Klabu ya Simba imetangaza kumsajili mshambuliaji Moses Phiri

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
1655323743577.png

Klabu ya Simba leo hii Juni 15, 2022 hatimaye imetangaza rasmi kumsajili mshambuliaji hatari Moses Phiri raia wa Zambia.

Phiri amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi akitokea klabu ya Zanaco FC ya nchini Zambia.

"Moses Phiri ni Mnyama, Karibu kwenye familia ya timu kubwa Afrika Mashariki na kati" imeeleza kwa ufupi taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wa Simba SC.

Mshambuliaji huyo hatari ambaye ametua Msimbazi kuongeza chachu katika eneo la ushambuliaji, amekuwa bora sana ambapo ndani ya misimu miwili ameweza kufunga mabao 27 kwenye Ligi Kuu ya nchini Zambia.
 
Kwani aziz ki mnamtambulisha lini sasa kama moses phiri mwenye dau dogo mumeshindwa je huyo aziz Ali wa mtongani mtamuweza kweli.
 
Tupeni wasifu wake kwanza.
Ni mchezaji mwenye kitu gani kipya tofauti na hawa wengine waliopo sasa?

Kamuangalie Youtube halafu njoo hapa, Kifupi strength ya Mguu wa Kushoto na Kulia Haina Tofauti, Body Fitness yake ni Ya juu sanaa, Akili yake ya Kufunga iko mbali sanaa, Ku drible mpira ndio kabisaaa

Kifupi wanahitajika akina Moses Phiri 2, Tukimchukua na Msuva, Basi Kagere Mugalu, Bocco na Kibu Denis Kwa heri
 
Bado mshambuliaji mwingine mkali kama Phili.

bado kiungo mkata kinyesi kama Lwanga/anatakiwa pale kati.

Tshabalala na show me the way wasaidiwe wale vijana washatumika sana wanaanza ku-flop.

Atafutwe center half mwingine wa uhakika alafu Inonga atumike namba nne,uchezaji wa namba tano wa Inonga kama mtu wa mwisho utaighalimu Simba huko mbeleni.

kocha wa viungo atafutwe mwingine injury za mara kwa mara shida ipo huko kwenye mazoezi ya viungo.
haya ni maoni tu wala sio lazima.
 
Back
Top Bottom