Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Klabu ya Simba leo hii Juni 15, 2022 hatimaye imetangaza rasmi kumsajili mshambuliaji hatari Moses Phiri raia wa Zambia.
Phiri amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi akitokea klabu ya Zanaco FC ya nchini Zambia.
"Moses Phiri ni Mnyama, Karibu kwenye familia ya timu kubwa Afrika Mashariki na kati" imeeleza kwa ufupi taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wa Simba SC.
Mshambuliaji huyo hatari ambaye ametua Msimbazi kuongeza chachu katika eneo la ushambuliaji, amekuwa bora sana ambapo ndani ya misimu miwili ameweza kufunga mabao 27 kwenye Ligi Kuu ya nchini Zambia.