Klabu ya Simba ni zaidi ya Vilabu vyote Afrika Mashariki, Historia na Kumbukumbu

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wadau msichoke bado tunaendelea kuleta Flashback kuhusu tulikotoka na tulipo sasa.

Simba ndo Klabu ya kwanza na ya pekee Tanzania, kufika nusu fainali klabu bingwa Afrika mwaka 1974.

Simba ndo Klabu ya kwanza na ya pekee Afrika kufungwa magoli 4-0 nyumbani na kwenda kushinda ugenini magoli 5-0 katika mashindano ya vilabu vya mabara dhidi ya Mufurila Wonderes ya Zambia mwaka 1979 mbele ya Rais Kenneth Kaunda.

Simba ndo klabu ya kwanza na ya pekee Tanzania kufika fainali Kombe la CAF mwaka 1993 fainali iliyopigwa uwanja wa Uhuru.

Simba ndo bingwa wa kwanza kwa klabu bingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1974 na mabingwa kwa ukata huu kwa mataji sita.

Simba ndo klabu ya kwanza kumfunga bingwa mtetezi Afrika Zamalek ya Misri na kumtoa kwenye michuano hiyo 2003.

Simba ndo klabu ya kwanza Tanzania kuvaa jezi Oktoba mwaka 1938 miaka miwili tangu kuanzishwa, huku mwaka 1951 wakiwa wa kwanza kuvaa viatu vya mpira.

Simba ndo klabu ya kwanza kupanda ndege mwaka 1960 walipoalikwa kwenye sherehe maalumu Ethiopia na King Haile Selassie.

Wekundu wa Msimbazi ndo wa kwanza kujenga jengo lake mwaka 1971, huku 1967 ikiwa ya klabu ya kwanza kununua basi kwa ajili ya wachezaji.

Wekundu wa Msimbazi wana Lunyasi ndo klabu ya kwanza kuwa bingwa wa Tanzania 1966 huku mwaka huu 2018 wakiwa na Mabingwa wa Nchi.

NB: Hakuna juu yake kwa Simba SC, This Is Simba Ghazwat sembo OKW BOBAN SUNZU King Ngwaba Shunie, Afrika Mashariki...Kama hujui unakotoka utajuaje unakwendaaa? Kazi Kwetu Wachanga na Wahenga katika Soka.

Watani zetu Klabu shindwa Mpo? Sibonike demigod Hajar kwa hisani Bunju de Stadium Karibu.
 
Ndo fimbo mnayotegemea hiyo kwa Rage. Tutawanyoosha mpaka usikie kichefuchefu, na hamuwezi kujibu hoja hizi zaidi maneno ya mipasho tu

si mmekaa na Kanjibai miaka kumi amefanya nini cha maana zaidi ya kujaza kifusi kwenye dimbwi la Vyura[emoji196][emoji196][emoji196]
Kweli nyinyi ni Mbumbumbu, Rage hakukosea hata kidogo.
 
Tutawanyoosha mpaka usikie kichefuchefu, si mmekaa na Kanjibai miaka kumi amefanya nini cha maana zaidi ya kujaza kifusi kwenye dimbwi la Vyura[emoji196][emoji196][emoji196]

Naleta nyingine hivi punde Vyura nyie[emoji196][emoji196]
Tuwavumilie mkuu hawa gongo wazi...
Hii historia wengine walikuwa hawaijui kwa hiyo lazima wapaniki!.
 
Nitajie walio na mipango zaidi kuliko Simba ili tujue.

Simba mipango wanayo ndo maana kwenye kuyatafuta mafaniko tumefikia hatua hizi za Klabu bingwa Afrika, Kombe la Caf kwa hatua hizo tajwa.
na ndiyo klabu bingwa kwa kupepesa 'domo' Africa, kelele nyingiiii, mipango sifuri, mafanikio sifuri....
 
Mk Mkuu, very impressive. Hizo record za kipekee zimezaa mataji mangapi?
Utashangaa kila mtu anajua Bingwa World Cup ni France. Wangapi watakuambia mshindi wa pili, wa tatu?
 

Mimi Nilijua tu Kuwa Post hii itamwaga Sumu katika Bwawa la Vyura! Unaona sasa wanavyotapatapa?

Wamebakia Kumwaga Mipasho tu
 
Mkuu mbona umepaniki?? Tatizo nini.. Au ndo ule mzimu wa mapasi zaidi ya 2341 unawaandama??

Unapimaje paniki hapo?

Mikia ni mabingwa wa porojo/mipasho na wizi.

Najaribu kuvuta picha majanga waliyoyapata viongozi wa mbumbumbu walioko rupango ingekuwa ndio yamewapata viongozi wa mabingwa wa kihistoria Yanga tungepigiwa taarab na nyinyi mikia mkiongozwa na yule msemaji wenu mwimba ngonjera hadi tukome.
 
Tulia wewe,mlichokuwa mnatamba kutoa draw na sisi ni nini.Kama ni timu ya kawaida mbona hamjutii kutoa draw na timu ya kawaida

Mbumbumbu ni mbumbumbu tu.

Mpira una matokeo matatu kushinda,kufungwa na kudraw.

Mumefungwa na Mbao Mkadraw na Ndanda na Yanga.

Rudini Uturuki mkaweke kambi upya.
 
Ulichoandika hapo ndo full porojo, nidhani utakuja na hoja kuntu kuwa mmefika hatua kadhaa kwenye michuano ya Afrika kuliko Simba..!

Lakini hata hivyo utatoa wapi zaidi ya kupayuka ooh viongozi wa Simba mara sijui mabingwa wa historia, hakuna habari hizo wewe!

Simba ndo bingwa wa nchi ya Tanzania, Kama hutaki kaogelee pale bwawani[emoji196][emoji196]
 
Mbumbumbu ni mbumbumbu tu.

Mpira una matokeo matatu kushinda,kufungwa na kudraw.

Mumefungwa na Mbao Mkadraw na Ndanda na Yanga.

Rudini Uturuki mkaweke kambi upya.
Turudi Uturuki kwanini? Kama mpira tumekufundisha unavyochezwa huku ukipumulia mashine kuomba mpira uishe.

Halafu kumbe Uturuki unawaumiza eeeh? Nini Uturuki Simba imeweka Kambi Brazil kwa wataalamu wa samba 1982
 
Mkuu still you are focusing on history hahahahaha you could die poor in life if you live with the history of your first grandpa money.....we live the present liverpool and man u zote zinahangaika maama zinaishi katika historia kuliko usasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…