Klabu ya Simba yamfungia Kessy

Klabu ya Simba yamfungia Kessy

Zile crosses alizopiga na kuzaa magoli tangu ajiunge Simba unajua ziko ngapi? Akifanya vyema, ni mchezaji mzuri, akikosea ni kirusi. Mpira ni mchezo wa makosa Mkuu, vumilieni.

Bao tulilofungwa na Mwadui FC ni dhahiri yalikuwa ni makosa binafsi ya Kamusoko lakini sisi hatujapiga kelele, mbona wenzetu hivyo au ndio Jerry Muro kawavuruga?
Kama ni kupiga hizo krosi ata Beckham alizipiga sana Man Utd lakini mwisho wa siku aliuzwa mpira ni zaidi ya krosi.
 
Kessy ni mchezaji mvumilivu sana!
Juzi baada ya mechi ya toto yule kipa bubu' alitandika ngumi za kutosha!
Muda wote wa mkataba simba ilikataa kutimiza vipengele kadhaa tena kwa maksudi kabisa ili kumkwaza tuu
Tangu kufungwa mechi ya yanga, mazoezin amekuwa akinyanyasika toka wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu

Hivi Polisi hawajaona kosa la jinai (Shambulio la mwili) dhidi ya huyo kipa wa Simba? Nilitegemea kusikia kawekwa ndani kwa kumpiga Kessy.

Nichukue fursa hii kumshauri Kessy aende Polisi akafungue RB ili huyo mtuhumiwa akamatwe na ashughulikiwe kwa mujibu wa Sheria. Hakuna mtu ndani ya Tanzania anayeruhusiwa kumpiga mtu mwingine. Mhe. Rais amekuwa akisisitiza kuheshimu sheria za nchi.
 
Simba yamfungia Hassan Kessy kutocheza mechi 5 kwa kumchezea rafu Christopher Edward wa Toto na kutolewa kwa kadi nyekundu, Haji Manara athibitisha.

===================

Klabu ya soka ya Simba imemsimamisha mchezaji wao Hassan Kessy Ramadhan mechi tano kwa kosa la kumchezea madhambi mshambuliaji wa Toto Africans Edward Christopher. Katika Mchezo uliochezwa April 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa Kessy alimchezea Christopher faulo, hivyo kupewa kadi nyekundu, na uongozi Simba umeamua kumfungia mechi hizo ili kupinga Vitendo vya Utovu wa nidhamu.

Kufungiwa mechi tano kwa Kessy maana yake ni kuwa amefungiwa hadi Mwisho wa msimu kwani Simba imebakisha mechi tano katika msimu huu. Hii inamaanisha kuwa Hassan Kessy Ramadhan si mchezaji tena wa Simba maana mechi tano alizosimamishwa ni sawa na mwezi mmoja ambao ni muda wa mkataba wake uliosalia.

Chanzo: Radio Free Africa
Kwanini msifukuze ol players
 
Mbona dogo tangu jana alishasema msimu ukiisha anahama timu
Na hatohudhuria mazoezi kuanzia sasa
 
Aende tu! Timu ilikuwa vizuri kwenye mechi na Toto.Yuko peke yake badala yakuondoa yeye anasubiri kumkanyaga mtu.Hii si nidhamu ya soka.Simba ni timu ya mfano hapa Tz,haipaswi kuwa na mtu asiyejua thamani yake ndani ya hii timu.
 
So bila maneno ya Muro ina maana Simba ingeshinda? Acheni kuwatupia lawama viongozi, mpira unachezwa na wachezaji
Mkuu mchezaji hata anapokuwa anafundishwa kunakuwa na somo la psychology kama hulijui hilo basi ndio ujue sasa
 
Japo kiwango na kipaji anacho, lakini hajui kwamba anachezea timu pekee yenye wachezaji ulaya.Simba inakuza vipaji vyenye nidhamu.Hivyo kama Yanga mnaona kaonewa msajilini tu hamna shida.Wapo wazuri kuliko yeye watapitia simba kwenda Ulaya.
 
Jerry Muro ni asset kubwa sana kwa Yanga, mdomo wake umefanikisha kuisamabaratisha Simba! Inanikumbusha kisa cha wana wa Israel kuuzunguka ukuta wa Yeriko kwa muda wa siku sita na siku ya saba ukuta ulianguka bila kuguswa na mtu yeyote.

Safi sana Jerry Muro, hakika umetusaidia sana kuimaliza Simba SC kwa maneno tu bila ya kuwapiga ngumi hata ya mgongoni!
Hongera sana mzee na huo ndio utani wa jadi wakati nyie kwenu ni kicheko sisi wenzenu ni masononeko,pia hongereni sana kwa kuwa na mtu kama jery muro kiufupi katumia nafasi yake vizuri sana
 
Muda si mrefu Manara atatuwekea historia ya Simba,kama uwanjani inacheza historia vile.
Mimi ni mwana msimbazi lkn huyu manara naona hii nafasi haiwezi,kwanza ni mtu mwepesi sana kum provoke
 
Haa haaaaaa. Hata mimi Nimemsifu sana murro kwa hili. Sasa Msimbazi kunawaka moto, wakati hakina mtu yeyote aliyeenda na kiberiti
Mkuu maneno ya muro ni ya kiweledi sana hasa yakikuta mtu ambaye uwezo wa kuyafanyia kazi ni mdogo kama manara,huwezi kuwa msemaji wa timu kubwa kama simba ukatawaliwa na hasira za hovyoooooooo
 
Simba ni Zaidi ya yeyote na Simba itaendelea kuwepo kama ambavyo ipo watu makini washaona mambo kwa jicho la tatu hawa madogo sijui kina Kessy wanarubuniwa ukweli huyu dogo anaigharimu sana Simba,ilifaa afukuzwe mapema sana sababu ni Kirusi ndani ya Klabu.
Mkuu naona unanitonesha vidonda,ila sasa sioni sababu ya kumpa lawama kesi kwani mbona washambuliaji hawakufunga goli likakataliwa?
 
Mkuu naona unanitonesha vidonda,ila sasa sioni sababu ya kumpa lawama kesi kwani mbona washambuliaji hawakufunga goli likakataliwa?
Mkuu Simba inatakiwa kusukwa upya kila Idara watoto wengi ninao waona hawako Makini, si katika safu ya Ushambuliaji tu ata viungo na zaidi Mabeki lazima watambue kila mechi ni muhimu lakini ukiangalia utoto ndio mwingi lazima viongozi nao wachukue hatua stahiki wakati wa kusajiri.
 
Mkuu Simba inatakiwa kusukwa upya kila Idara watoto wengi ninao waona hawako Makini, si katika safu ya Ushambuliaji tu ata viungo na zaidi Mabeki lazima watambue kila mechi ni muhimu lakini ukiangalia utoto ndio mwingi lazima viongozi nao wachukue hatua stahiki wakati wa kusajiri.
Sawa ndugu yangu lkn ujue huu sasa ndio tunafunga mwaka wa tano hatujui ubingwa na bado tunaendelea kutoa excuse kwa viongozi wetu huoni kuwa sasa ni muda muafaka tukawageukia kina dalali?
 
njoo Jangwani Kessy uokoe kipaji chako....


halafu vipi na isihaka si na yeye ana utovu wa nidhamu...vp wadau wa nyau sc hamumtemi nae? maana hii ndo fursa nzuri ya kujipatia wachezaji wenye vipaji bila kutumia hata nguvu nyingi wala gharama kubwa, maneno ya jerry tu yanatosha
 
njoo Jangwani Kessy uokoe kipaji chako....


halafu vipi na isihaka si na yeye ana utovu wa nidhamu...vp wadau wa nyau sc hamumtemi nae? maana hii ndo fursa nzuri ya kujipatia wachezaji wenye vipaji bila kutumia hata nguvu nyingi wala gharama kubwa, maneno ya jerry tu yanatosha
Kwa hilo mmelamba dume,jery ni kiboko ya manara hiyo haina ubishi
 
Back
Top Bottom