Klabu ya Simba yathibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama

Klabu ya Simba yathibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama

Mayele alimtoboa Juma kaseja pale Taifa akiwa anacheza timu ya Taifa ya Kongo. Ukiacha Samata na Msuva hakuna forward wa kibongo mwenye Kariba ya Mayele Kwa Sasa.
Ni kwasababu ya Chupri za Marefa ndio maana alikosa kiatu Cha mfungaji Bora ila hakuna mshabiki asiyejua ukweli kuhusu uwezo wa Mayele.
Hata Mpole mwenyewe analijua hilo...
 
Klabu ya Simba, Wekundu wa Msimbazi leo Julai 11, 2022 imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Kagera Sugar.

Nyota huyu msimu uliopita akiwa na Kagera Sugar, alikuwa na wakati nzuri huku akifunga mabao 2 na assist 3 katika michezo 25 huku akicheza nafasi tofauti tofauti ndani ya uwanja, ambapo muda mwingine alicheza nafasi ya mlinzi wa kati, hali iliyoivutia benchi la ufundi la Simba SC kumsajili.

"Kipaji kikubwa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Tanzania, kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu, Nassoro Kapama ni Mnyama". Imeeleza hivyo Taarifa ya Simba SC

View attachment 2287078
Kapama huyu aliye cheza mpaka na kina nsajigwa au mwingine
 
Klabu ya Simba, Wekundu wa Msimbazi leo Julai 11, 2022 imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nassoro Kapama kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Kagera Sugar.

Nyota huyu ambaye ni Kiraka ndani ya dimba, ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili, eneo la Kiungo cha mshambuliaji, Kiungo cha ulinzi, eneo la ulinzi wa katikati huku akiwa amefunga mabao 2 na assist 3 katika michezo 25, akiwa na Klabu ya Kagera Sugar.

"Kipaji kikubwa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Tanzania, kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu, Nassoro Kapama ni Mnyama". Imeeleza hivyo Taarifa ya Simba SC

View attachment 2287078
Ohoo sisi wenzetu Alhly ,tunasajili level za Alhly, maneno mengi........ okay hongera Kapama, je wana Simba mtamvumilia kama akiwa chini ya kiwango,manake sisi washabiki wabongo hatunaga uvumilivu.

Kama kwaida yetu usajili wanafanya viongozi lawama atapewa kocha, tuna safari ndefu na mpira wetu.
 
Fundi saana huyu mtu, sijui kwanini alikuwa anacheza beki, ni kiraka haswaa, naanza kumuona alikuwa ni kiungo, anapiga mpaka 10 mixer kiungo wa chini..

Kigamboni, kuna vipaji saana, hapo umkute VIDUKA kapiga majimaji nadhani msimu mmoja tu, kuangalia kwangu ndondo koote sijaona fundi kama huyu mtu, ni ana akili ya mpira, kumtizama ni burudani saana,
Kuna TUGA huyu sijui uchawi ninj kwenye ubora wake anafaa kabisa kucheza preme, sijui ndio bahati hana

Na wengine weengi.
 
Wachache sana wenye kuelewa hilo

Klabu ya Simba SC msimu huu umeamua kujitenga na mihemko, inasajili kwa mahitaji.
 
Nyota huyu ambaye ni Kiraka ndani ya dimba, ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili, eneo la Kiungo cha mshambuliaji, Kiungo cha ulinzi, eneo la beki wa katikati huku akiwa amefunga mabao 2 na assist 3 katika michezo 25, akiwa na Klabu ya Kagera Sugar, hali iliyoivutia benchi la ufundi la Simba SC kumsajili.
Tumepigwa hapa aisee, Simba sijui kwa nini tunasajili kwa mihemko

Huyu dogo ataenda kusugua benchi pale naona maana hao wa kimataifa ndio watachukua nafasi yake
 
Makolo mlienda fifa kabisa au umesahau?
Kwenda FIFA ni suala ambalo lipo kiseria kwa vile ndo chombo kinachosimamia mpira duniani.

Wajinga ni wale waliotaka kwenda Ikulu kumuona Rais Samia kumpelekea mambo ambayo kwenye nchi anayoiongoza vipo vyombo vya kusimamia hayo.
 
Screenshot_20220711-122608_Instagram.jpg
 
Simba inazidi kujiimarisha kwa wachezaji wa uhakika siyo wenzetu wanaowachukua wachezaji walioisha mpk kuwa wabeba mizigo store
Ila Hersi kawafanya kitu mbaya Utopolo hadi huruma,bora angemleta kimya kimya tu lakini zile tambo zake hadi kumtumia kama kifaa chake cha kampeni ndiyo imepelekea watu waingie chimbo hadi kujua kumbe alishaacha kucheza kitambo tu.
 
Back
Top Bottom