Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 16,074
- 27,490
Sina ushabiki maandazi wa kuchoma jezi ila kwa hili lazima wawajibike waliohusika. Sitonunua jezi wala sitakwenda uwanjani kuishabikia timu yangu. Naamini wapo wengine wengi waliochukizwa na hili.Msiharibu mali za club, msichome moto jezi zenu kuonesha hasira na kutokubaliana na kilichofanyika.. Klabu yenu ni nzuri sana ikikaa mbali na wanasiasa.. Michezo ni furaha.. Siasa ni fadhaa!
Kuna watu wana support kilichofanyika! Nimegundua ni mbogamboga ndani ya clubSina ushabiki maandazi wa kuchoma jezi ila kwa hili lazima wawajibike waliohusika. Sitonunua jezi wala sitakwenda uwanjani kuishabikia timu yangu. Naamini wapo wengine wengi waliochukizwa na hili.
Naungana na wewe ndugu. Morali imekata ghafla viongozi wameinajisi klabu na sisi mashabiki hatuna PAWA tena.Hizo conspiracies hatuzijui. Tunachojua Rais wa klabu kaiwakilisha klabu kutoa mchango wa milioni 100. Mashabiki na wanachama imetukwaza. Propaganda za yanga kushiriki kupigania uhuru ni upumbavu tu. Tumeipenda yanga kwa sababu za kimpira sio za kisiasa. Binafsi morali ya kuelekea msimu mpya imeshuka sana. Bila viongozi kujitokeza kuomba radhi siwezi kutoa ushirikiano wowote wa kishabiki kwa hii timu.
Hao ndio washenzi wasiojua madhara ya kuchanganya mpira na siasa. In real sense kwa hili watawajibika wote waliotufanya mazumbukukuKuna watu wana support kilichofanyika! Nimegundua ni mbogamboga ndani ya club
Basi na sisi wana Chadema,Act,Nccr tulioko Yanga mnachangia lini vyama vyetu. Yanga si ya wana CCM tu hilo ni kosa la kiufundi siasa itavunja club zetu. Michango ya ukombozi 1957 kwa TANU ni mazingira tofauti na sasa tuwe makini. Pesa zetu zirudishwe haraka.Muda Sio Rafiki Kwasasa!
Barua Zimesha-jam Kwenye ethics@fifa.org
utetezi wowote kwasasa inatakiwa upitie huko.
1957 kilikua chama cha ukombozi sio siasa.Basi na sisi wana Chadema,Act,Nccr tulioko Yanga mnachangia lini vyama vyetu. Yanga si ya wana CCM tu hilo ni kosa la kiufundi siasa itavunja club zetu. Michango ya ukombozi 1957 kwa TANU ni mazingira tofauti na sasa tuwe makini. Pesa zetu zirudishwe haraka.
Hersi huwa hahitaji mweka hazina, anamruka tu kama kwenye usajili. Wadhamini wana mikataba yao. Hapo ilikuwa ni weledi, busara na hekima za HersiNa je body ya wadhamini wanajua? Mweka hazina je!?
Kuna maneno yamekatwa hapo sikiliza hiiWatu wabad balaa.Kalishwa maneno
πππRais wao anasimama anasema sisi kama yanga tumechangia 100M arf unakuja kupinga ,ndg mwandishi unabisha Nini Kwan ww ulikuwepo?
Yeye ni Rais wa vilabu Africa. "Mimi ni SIMBA damu najuikana hivyo.. Na kama mtani wa jadi wa Yanga! Inapopata madhila nafurahi.. Ila kwa hili la kuchangia million mia moja nawatetea hawajafanya hivyo
Vilabu vyetu hivi vya soka vingi vinaongozwa na wafadhili na wadhamini, hawana vyanzo vya uhakika vya kuwaingizia mapato binafsi kama wao
Kilichotokea kwenye ile harambee ni michezo michafu ya kisiasa kupitia makundi yanayosigana kuelekea uchaguzi mkuu ili kuonesha kuungwa mkono kwenye kila kaliba
Kundi maarufu la wanamtandao waliopewa jina la wahuni ndio wamecheza mchezo huo mchafu kupitia kada wa CCM ambaye pia ni rais wa YANGA.
Huyu kwa kujua ama la akatwishwa zigo la kutangaza kiwango tajwa kuwa kimechangwa na Yanga (Young African Sports Club)
Nina hakika hakuna mwana Yanga kupitia viongozi wao aliyeshirikishwa kwenye hili.. Wote walishangaa tu kama wengine
Rai yangu kwa wana Yanga
Msiharibu mali za club, msichome moto jezi zenu kuonesha hasira na kutokubaliana na kilichofanyika.. Klabu yenu ni nzuri sana ikikaa mbali na wanasiasa.. Michezo ni furaha.. Siasa ni fadhaa!
Jipangeni mshikamane mumuwajibishe rais wenu! Huyu ndiye mchawi wenu.. Mumbane kupitia njia sahihi aseme alipata wapi hizo hela na ni nani alimpa mamlaka ya kuihusisha klabu na harambee ya kisiasa
Kwenye hili sisi SIMBA tunaweza kushirikiana nanyi kukomesha tabia hii mbovu ya wanasiasa wachovu kuvitumia vilabu vyetu kwa maslahi binafsi
Sisi SIMBA tunaojitambua tuko na Wana Yanga wote waliokasirishwa na tukio la harambee na tutakuwa nao bega kwa bega mpaka wanasiasa wakae mbali na michezo