Kleist sykes (1894 - 1949) katika dictionary of african biography (dab) oxford university press, n

Kleist sykes (1894 - 1949) katika dictionary of african biography (dab) oxford university press, n

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074

DSCN1129.JPG


DSCN1154.JPG


Wanaukumbi,
Naweka hapa vipande kutoka Dictionary of African Biography (DAB) ambao ni mkusanyo kwa njia ya maandishi ya Waafrika walioacha alama katika maendeleo ya bara hili.
Huu ulikuwa mradi wa Oxford University Press (OUP) na Chuo Cha Harvard na ulichukua miaka kadhaa kukamilika. Nilikuwa mmoja wa waandishi waliotakiwa kuwaandika baadhi ya Watanzania na Watanganyika waliofanya makubwa katika historia ya nchi yao. Mradi huu ulikuwa chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong wa Harvard na ulikusanya waandishi 500 kutoka Afrika na kwengineko. Nilimshauri Prof. Akyeampong akate baadhi ya majina kwa kuwa kwa hakika hawakuwa na mchango wowote wa maana isipokuwa labda baadhi walipata kuwa na vyeo katika serikali. Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatika ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao.

OUP wametoa volume sita za kazi hii mwaka 2011. Volume hizi sita zinauzwa USD 1300 na vilevile zinapatikana kwenye mtandao kwa subscribers. Nimeletewa ukurasa ulio na makala niliyoandika kuhusu maisha ya Kleist Sykes (1894 - 1949) nami nimeona itakuwa vyema kama nitaweka hapa vipande vipande ili wasomaji wasome kwa faida ya kuhifadhi kumbukumbu za wazee wetu. Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatika ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao. Labda msomaji utataka kujua kwa nini nilichagua kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.

Nimemchagua Kleist Sykes kwa sababu hizi kubwa:



  • [*=left]Kwanza alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Asociation mwaka 1929 na muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 akiwa katibu vilevile na kwa jinsi siasa za kiloloni zilivyokuwa wakati ule za ''wagawe uwatawale,'' yeye aliunganisha vyama hivi katika uongozi mmoja lau kama Al Jamiatul Islamiyya kilikuwa chama cha Waislam na wakati huo huo akaweza kuweka misingi ya kuwashirikisha Wakristo katika kupigania haki za Mwafrika wa Tanganyika katika African Association.


  • [*=left]​
    [*=left]Pili Kleist alifungua mlango wa Waislam wawe na shule zao wenyewe ili kukabiliana na shule za Wamishionari ambazo zilikuwa zikiwabatiza watoto wa Kiislam katika shule zao na hili liliwafanya wazazi wa Kiiislam kusita kuwapeleka watoto wao shule.

    [*=left]

    [*=left]Tatu katika kutimiza hili alianzisha shule ya Kiislam - Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ambayo ilisomesha masoma ya kisekula na Qur'an. Inasemekana ilikuwa ndoto ya Kleist kuona Qur'an inasomeshwa kwanye madawati na wanafunzi wamekaa katika viti kama shule badala ya zile madras za asili ambazo watoto wanakaa chini katika majamvi. NIa yake ikiwa kuwa katika shule mtoto atapata yote mawili - elimu ya dini yake na masomo ya kisekula. Ndoto hii ya Kleist sasa si ndoto tena kwani shule za Kiislam nyingi zimeanzishwa nchini pote miaka mingi baada ya yeye kutangulia mbele ya haki zikisomesha Qur'an na masomo ya kisekula kwenye darasa moja na mwalimu akiwa kasimama mbele ya ubao.

    [*=left]

    [*=left]Jambo la nne ni lile la kuuweka wazi mlango wa TANU kwa Wakristo ambao wakati wa vuguvugu la kuanzisha African Association mwaka 1929 serikali iliwatisha wasijiunge na chama hicho.

TANU ilipokuja asisiwa na mwanae na wazalendo wengine mwaka 1954 hali ilikuwa haijabadilika lakini uongozi wa Waislam ndani ya TANU uliweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa TANU haivurugwi na hisia za Uislam kiasi cha kuwaweka pembeni ndugu zao Wakristo. Hii ndiyo sababu ikawezekana Nyerere kuchaguliwa kuongoza TAA mwaka 1953 na TANU ilipokuja asisiwa 1954 haikuwa tabu kwake yeye kukabidhiwa jukumu la kuwaunganisha Waafrika chini ya bendera moja ya kudai uhuru.

Hizi ndizo sababu nne zilizonipelekea kuandika maisha ya Klesit Sykes katika Dictionary of African Biography.

DSCN1135.JPG





DSCN1131.JPG



DSCN1132.JPG


DSCN1138.JPG


DSCN1137.JPG



DSCN1141.JPG



DSCN1140.JPG



DSCN1142.JPG
 
Ahsante mkuu kwa historia hii fupi.
 
Why kina Sykes wanapenda mno kujiita Sykes wakati jina lao ni Mbuwane?
hata wajukuu zao utasikia Adams Sykes au Abraham Sykes....

unaweza fikiri ni wazungu wakristo

kumbe wengi ni waislam waswahili......

what are they so hard trying to achieve?
 
imenifumbua macho kwenye mambo mengi sana, thanks mkuu
 
Why kina Sykes wanapenda mno kujiita Sykes wakati jina lao ni Mbuwane?
hata wajukuu zao utasikia Adams Sykes au Abraham Sykes....

unaweza fikiri ni wazungu wakristo

kumbe wengi ni waislam waswahili......

what are they so hard trying to achieve?

Au Araf sykes.....nadhani ukweli wa kuwa baba yake kleist alikuwa ZULU mercenary, tayari na wao wanajiona wa sauz, ila wanasahau kuwa yule alikua anaitwa Sykes Mbuwane...sasa kwasababu Mbuwane limekaa ki local zaidi na haya mambo ya dotcom na mauzungu mengi, sykes ndo jina waliloliona liko safi zaidi mkuu.
 
Au Araf sykes.....nadhani ukweli wa kuwa baba yake kleist alikuwa ZULU mercenary, tayari na wao wanajiona wa sauz, ila wanasahau kuwa yule alikua anaitwa Sykes Mbuwane...sasa kwasababu Mbuwane limekaa ki local zaidi na haya mambo ya dotcom na mauzungu mengi, sykes ndo jina waliloliona liko safi zaidi mkuu.

Ajabu sana
Familia iliyopigania sana waislam na waswahili inajaribu so hard
kuwa mbali na image ya 'uislam na uswahili'
wanaji portray kama wakristo walio na western culture zaidi
 
Ajabu sana
Familia iliyopigania sana waislam na waswahili inajaribu so hard
kuwa mbali na image ya 'uislam na uswahili'
wanaji portray kama wakristo walio na western culture zaidi

tatizo la kizazi cha dotcom mkuu. Badala ya kujali na kuendeleza legacies za waliowatangulia, zinatupilia mbali hayo na kuenzi mambo ya ajabu.
 
Nikupongeze kwa andiko lako!! Lakin ukisoma kwa jicho la tatu I mean between lines.. kuna upungufu ambao uko wazi ama umefanya makusudi kwa kuwa bias ama unataka kupotosha umma!!! Kwanza unataka kutuaminisha kwamba TAA malengo yake yalikuwa ni kudai uhuru so kilikuwa chama cha kisiasa... Pili kuchaguliwa kwa Nyerere kuwa Mwenyekiti wa TAA mkristo ilikuwa n hisani na si uwezo binafsi wa Nyerere... Tatu hutaki kutambua mchango binafsi wa Nyerere wa kubadilisha malengo ya TAA na kuunda TANU kama chama cha siasa... Sisemi Sykes hakuwa na mchango la hasha alikuwa na mchango mkubwa sana... Lakini tatizo la andiko lako limejaa ushabki na msukumo wa kiimani ambao unapelekea kupotosha ukweli ili mradi tu umjaze mtu sifa hata kama hakuwa nazo!!!
 
Back
Top Bottom