Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wanaukumbi,
Naweka hapa vipande kutoka Dictionary of African Biography (DAB) ambao ni mkusanyo kwa njia ya maandishi ya Waafrika walioacha alama katika maendeleo ya bara hili. Huu ulikuwa mradi wa Oxford University Press (OUP) na Chuo Cha Harvard na ulichukua miaka kadhaa kukamilika. Nilikuwa mmoja wa waandishi waliotakiwa kuwaandika baadhi ya Watanzania na Watanganyika waliofanya makubwa katika historia ya nchi yao. Mradi huu ulikuwa chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong wa Harvard na ulikusanya waandishi 500 kutoka Afrika na kwengineko. Nilimshauri Prof. Akyeampong akate baadhi ya majina kwa kuwa kwa hakika hawakuwa na mchango wowote wa maana isipokuwa labda baadhi walipata kuwa na vyeo katika serikali. Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatika ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao.
OUP wametoa volume sita za kazi hii mwaka 2011. Volume hizi sita zinauzwa USD 1300 na vilevile zinapatikana kwenye mtandao kwa subscribers. Nimeletewa ukurasa ulio na makala niliyoandika kuhusu maisha ya Kleist Sykes (1894 - 1949) nami nimeona itakuwa vyema kama nitaweka hapa vipande vipande ili wasomaji wasome kwa faida ya kuhifadhi kumbukumbu za wazee wetu. Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatika ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao. Labda msomaji utataka kujua kwa nini nilichagua kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.
Nimemchagua Kleist Sykes kwa sababu hizi kubwa:

[*=left]Kwanza alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Asociation mwaka 1929 na muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 akiwa katibu vilevile na kwa jinsi siasa za kiloloni zilivyokuwa wakati ule za ''wagawe uwatawale,'' yeye aliunganisha vyama hivi katika uongozi mmoja lau kama Al Jamiatul Islamiyya kilikuwa chama cha Waislam na wakati huo huo akaweza kuweka misingi ya kuwashirikisha Wakristo katika kupigania haki za Mwafrika wa Tanganyika katika African Association.
[*=left]​
[*=left]Pili Kleist alifungua mlango wa Waislam wawe na shule zao wenyewe ili kukabiliana na shule za Wamishionari ambazo zilikuwa zikiwabatiza watoto wa Kiislam katika shule zao na hili liliwafanya wazazi wa Kiiislam kusita kuwapeleka watoto wao shule.
[*=left]
[*=left]Tatu katika kutimiza hili alianzisha shule ya Kiislam - Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ambayo ilisomesha masoma ya kisekula na Qur'an. Inasemekana ilikuwa ndoto ya Kleist kuona Qur'an inasomeshwa kwanye madawati na wanafunzi wamekaa katika viti kama shule badala ya zile madras za asili ambazo watoto wanakaa chini katika majamvi. NIa yake ikiwa kuwa katika shule mtoto atapata yote mawili - elimu ya dini yake na masomo ya kisekula. Ndoto hii ya Kleist sasa si ndoto tena kwani shule za Kiislam nyingi zimeanzishwa nchini pote miaka mingi baada ya yeye kutangulia mbele ya haki zikisomesha Qur'an na masomo ya kisekula kwenye darasa moja na mwalimu akiwa kasimama mbele ya ubao.
[*=left]
[*=left]Jambo la nne ni lile la kuuweka wazi mlango wa TANU kwa Wakristo ambao wakati wa vuguvugu la kuanzisha African Association mwaka 1929 serikali iliwatisha wasijiunge na chama hicho.
TANU ilipokuja asisiwa na mwanae na wazalendo wengine mwaka 1954 hali ilikuwa haijabadilika lakini uongozi wa Waislam ndani ya TANU uliweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa TANU haivurugwi na hisia za Uislam kiasi cha kuwaweka pembeni ndugu zao Wakristo. Hii ndiyo sababu ikawezekana Nyerere kuchaguliwa kuongoza TAA mwaka 1953 na TANU ilipokuja asisiwa 1954 haikuwa tabu kwake yeye kukabidhiwa jukumu la kuwaunganisha Waafrika chini ya bendera moja ya kudai uhuru.
Hizi ndizo sababu nne zilizonipelekea kuandika maisha ya Klesit Sykes katika Dictionary of African Biography.