Klopp aelezea sababu ya mchezo wa Liverpool na Man United kuwa mgumu

Klopp aelezea sababu ya mchezo wa Liverpool na Man United kuwa mgumu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mchezo wetu (Liverpool) ugenini dhidi ya Manchester United ni mechi maalum kwa United kuliko wanapocheza dhidi ya timu nyingine, wanacheza kwa bidii zaidi ya kawaida yao, ndio maana inakuwa mechi ngumu, hivyo ndivyo ilivyo.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, Aprili 7, 2024, ametoa kauli hiyo baada ya matokeo ya magoli 2-2 ya timu yake dhidi ya Manchester United katika Premier League, akielezea sababu kwa nini mchezo baina ya timu hizo huwa unakuwa mgumu kwake hata kama United haina kiwango kizuri.

Rekodi za Liverpool ya Klop dhidi ya Man United ikiwa chini ya Kocha Erik ten Hag:

Robo Fainali FA Cup (Machi 17, 2024)
Man United 4-3 Liverpool

EPL (Desemba 12, 2023)
Liverpool 0-0 Man United

EPL (Machi 5, 2023)
Liverpool 7-0 Man United

EPL (Agosti 22, 2022)
Man United 2-1 Liverpool

Kirafiki (Julai 12, 2022)
Man United 4-0 Liverpool
 
Watanzania Baada ya kujifunza mpira duniani

Wao wamekazana na simba na yanga tu, majadiriano yao kila kona ni simba na yanga sijui nani amewaroga.

Masokoni, stendi, Daladala, vijiwe vya kahawa nk.

WATANZANIA KUWENI NA AKILI
 
hiyo game liver baada ya kuongoza alibweteka tu....hakupambana kama mtu anaesaka ubwinga.

Eliot amejitahidi sana yule dogo..game changer.
 
hiyo game liver baada ya kuongoza alibweteka tu....hakupambana kama mtu anaesaka ubwinga.

Eliot amejitahidi sana yule dogo..game changer.
Liva alitakiwa kumaliza mechi first half hata ile game ya fa alipigwa kwa uzembe huo huo ile mechi alitakiwa kuimaliza kabla Antony hajachomoa dakika za mwisho.
 
Back
Top Bottom