KMC FC Vs Simba SC (0-2) | Dimba la Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

KMC FC Vs Simba SC (0-2) | Dimba la Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League (VPL) Kuendelea kupigwa leo July 7, 2021 ambapo Kinondoni Municipal KMC FC, wanawakabili Mabingwa wa Nchi Simba SC, kwenye Dimba la Mkapa Jiji Dar es salaam.

KMC FC wanaingia Dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza, hivyo kwa upande wao wanasema wanaingia na mbinu nyingine ya kutofungwa huku Simba SC wakisema wanazitaka alama tatu ili kujiweka karibu kabisa na Ubingwa.

Kocha wa KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa "Simba SC walitufunga mchezo wa kwanza haijalishi wamekuja kupoteza mchezo wao uliopita pia, lakini sisi tunatengeneza mbinu zetu ili wasitufunge mchezo wa kesho (leo)". Amesema Kondo.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi Suleiman Matola amesema "Maandalizi kwenye mchezo wa kesho (leo) yamekamilika kwa kiasi kikubwa huku matumaini ya ushindi yakiwa makubwa.

Mchezo utakuwa mgumu kwasababu Ligi inaelekea ujingoni na kila timu inataka kumaliza ikiwa katika nafasi nzuri, sisi tunataka ubingwa na tunaamini tutaondoka na alama tatu muhimu". Amesema Matola.

Yote kwa Yote dakika 90 za jasho na damu kuamua.. Usikose Ukasimuliwa..Kumbuka mchezo huu ni kuanzia saa 1:00 Usiku

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....Ghazwat....
Probably kikosi
Ally Salim
Kapombe
J.kenedy
Wawa
Lwanga
Ndemla
Chama
Miraji
Miqsone
Bocco
 
Utopolo Walikuwa hawatii mguu Kwenye nyuzi Kama hizi, Sasa Wamepata nguvu Wapo wengi humu......!
KMC anakufa muendelee Kuwepo humu...!
 
Nawatakia kila heri Simba ili muweze kuchukuwa ubingwa mliohangaikia toka ligi inaanza. Lakini benchi la ufundi kuanzia leo lianze kuwatumia Dilunga na Ndemla hata kwa dakika chache ili ikifika siku ya fainali ya FA Kigoma wawe tayari kwa mapambano. Ikiwa kuna ulazima wa Morison kutumika awe anaanzia benchi halafu aingie zikiwa zimebaki dakika 30/20 za mwisho na pia aelezwe aache utoto na ubinafsi wa kukaa na mpira muda mrefu akitaka afunge peke yake wakati timu ina wachezaji 11 uwanjani. Na ajifunze kukaba badala ya kutembea uwanjani wakati amenyang'anywa mpira.
 
Watakuwa wamehaidiwaa kitu[emoji1787][emoji1787]
 
02' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Chama

KMC FC 0-1 Simba SC
 
Back
Top Bottom