KNCHR yavunja ukimya kuhusu Twaha Mwaipaya: Kenya yaonywa isigeuke kituo cha utekaji wa Wanaharakati

KNCHR yavunja ukimya kuhusu Twaha Mwaipaya: Kenya yaonywa isigeuke kituo cha utekaji wa Wanaharakati

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu Kenya (KNCHR) imeibua wasiwasi kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Salim Mwaipaya, na kuonya kuwa Kenya haipaswi kutumiwa kama eneo la utekaji, watu kutoweshwa kwa lazima au kuhamishwa kuvuka mipaka kinyume cha sheria.

Katika taarifa ya Oktoba 29, 2026, tume hiyo imesema Mwaipaya alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos, Oktoba 25, alipokuwa akisafiri kwa teksi kwenda kuwatembelea marafiki. Kwa mujibu wa taarifa ambayo tume ilipokea, Twaha alilazimishwa kutoka ndani ya gari na kuchukuliwa na watu waliokuwa kwenye msafara wa magari matatu.

Aidha KNCHR imefichua pia kuwa Mwaipaya alikimbilia Kenya mwaka 2025 akihofia maisha na usalama wake nchini Tanzania. Tume hiyo sasa inaitaka Serikali ya Kenya kubaini aliko Twaha haraka, kuhakikisha usalama wake na kuwawajibisha wote watakaopatikana kuhusika na kutekwa kwake.

Tume hiyo pia imeliweka tukio la utekaji wa Twaha Mwaipaya katika muktadha mpana wa visa vya kutekwa na kutoweshwa kwa watu wanaotafuta hifadhi au wanaohusishwa na upinzani wa kisiasa katika ukanda huu na kusisitiza kuwa Kenya ina wajibu wa kikatiba na kimataifa kulinda haki za kila mtu aliye ndani ya mamlaka yake, bila kujali uraia au hadhi yake ya uhamiaji.

Je, Kenya inaweza kuendelea kujitambulisha kama kimbilio la wanaokimbia mateso ya kisiasa ikiwa usalama wao ndani ya nchi unatiliwa shaka?

Soma pia
 

Attachments

  • 3162.jpeg
    3162.jpeg
    140.5 KB · Views: 9
  • 3163.jpeg
    3163.jpeg
    91 KB · Views: 9
Back
Top Bottom