Knesset yaidhinisha Mswada wa kunyonga wafungwa wa Kipalestina

Knesset yaidhinisha Mswada wa kunyonga wafungwa wa Kipalestina

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Knesset ya Israel imepitisha kwa usomaji wa kwanza mswada unaoruhusu kunyongwa kwa wafungwa wa Kipalestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Israel (KAN), mswada huo ulipitishwa Jumatatu usiku kwa kura 39 za ndiyo na 16 za hapana.

Mswada uliopendekezwa na chama cha Jewish Power cha Waziri wa Usalama wa Taifa Itamar Ben-Gvir, unataka mtu yeyote atakayemuua raia wa Israel kwa chuki au nia ya kuidhoofisha nchi hiyo, ahukumiwe kifo bila kupunguziwa adhabu.

Ben-Gvir alisherehekea hatua hiyo kupitia X akisema, “Jewish Power imeandika historia.”

Mashirika ya haki za binadamu yamepinga vikali mswada huo, yakionya kuwa unawalenga Wapalestina na kuongeza ubaguzi.

Kupitishwa kwa mswada huo kunakuja wakati Wapalestina wanakabiliwa na athari za vita vya Israel dhidi ya Gaza na mashambulizi yanayoendelea katika Ukingo wa Magharibi, huku zaidi ya wafungwa 10,000 wa Kipalestina wakiripotiwa kuteseka magerezani.

 
Ben Gvir ameendesha campaign za miswaada ya kuwanyonga wapalestina Toka miaka 20 iliyopita ....Huyu Mzee siku ambayo atachaguliwa kuwa waziri mkuu nahisi atapiga nuclear Iran na hapo gaza
 
💥Kurushwa katika Knesset: Muswada wa adhabu ya kifo kwa magaidi wapitishwa kusomwa kwanza

Muswada unaowezesha adhabu ya kifo kwa magaidi waliohukumiwa kwa mauaji ulipitishwa kusomwa kwa mara ya kwanza jana usiku huku wabunge 39 wakipiga kura ya kuunga mkono na 16 wakipinga.

Wakati wa kura, kulikuwa na mapigano makali katika ukumbi wa kikao; usalama ulilazimika kuingilia kati ili kuwatenganisha kiongozi wa chama cha Kiarabu Ayman Odeh na Waziri wa Polisi Itamar Ben-Gvir.

Baada ya kura, Ben-Gvir alisambaza baklava, ishara inayodhihaki desturi ya Wapalestina ya kusambaza pipi katika kusherehekea mashambulizi mabaya ya kigaidi dhidi ya Waisraeli, na kutangaza kwa dhati:

"Hii itakuwa sheria muhimu zaidi katika historia ya Taifa la Israeli."

Muswada huo unasababisha mijadala mikali ndani na kimataifa, kati ya wale wanaouona kama njia ya haki na kuzuia, na wale wanaoonya kuhusu mmomonyoko wa kanuni za msingi za utawala wa sheria.
 

Attachments

  • IMG_7749.MP4
    918.2 KB
Nchi za kiarabu pia zinanyonga watu hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom