Nimeishi Marekani tokea mwaka 2000. Makazi yangu yamekuwa Southern California ambayo inajumuisha San Diego na jiji kubwa la pili kuliko yote USA la Los Angeles. Tokea nikiwa secondary Tanzania nilikuwa mpenzi wa mpira wa kikapu (basketball). Kwa hio nilivyofika USA na sababu maskani yalikuwa Southern Caifornia, ni wazi kwamba ushabiki wangu ulielekea kwa Los Angeles Lakers. Enzi hizo ni Kobe Bryant ndio alikuwa anatesa sana. Team yake ya LA Lakers ilitisha sana na kushinda NBA championships mwaka wa 2000, 2001, na 2002. Kobe Bryant alishinda tena NBA World Championships mwaka wa 2009 na 2010. Kweli sikufanikiwa kwenda kuona mechi live sababu ya majukumu mengi mtu ukiwa nchi za watu. Lakini nilikuwa naangalia mechi sana muda mwingi kupitia runinga na LA Lakers wakishindwa roho ilikuwa inauma.
Leo nilivyopata habari za kifo cha champion KB anayefahamika kwa jina la Black Mamba sababu alitesa watu kama vile nyoka wa black mamba anayomwaga sumu na kukumaliza mara moja, niliumia sana sababu nimekuwa nikimfuatilia mchezaji huyo sana na alitupatia burudani ya nguvu sana mashabiki wa mpira wa kikapu.
Kobe Bryant amefariki akiwa na utajiri mkubwa zaidi ya ule wa Bakhresa au wa Mengi. Thamani yake ni US$500 million katika kifo chake. Hiyo inaonyesha mali si kitu, wote tutaelekea tu huko. Huwa jamaa hata akienda kufanya mazoezi kwa gym ya LA lakers au kwenda Staples center uwanja wa kikapu kucheza, alikuwa anasafiri na hellicopter tu. Huwa hachukuagi gari jamaa hata kama sehemu sio mbali. Kweli inasikitisha sana kwamba usafiri alioupenda sana ndio umemuua. Mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 anayeitwa Gianna amefariki pia. Chanzo cha ajali hio kinafanyiwa utafiti.
RIP Black Mamba!
Aina ya hellicopter iliyomuua KB24 Kobe Bryant akiwa na mwanae Gianna ambaye pia amefariki leo. Watu wengine watatu wamefariki pia katika ajali hio ya hellicopter.
Picha ya ajali hio
Njia ya hellicopter iliyoanguka
mwanamichezo nyota wa mpira wa kikapu nchini marekani katika ligi maarufu ya nba amefariki pamoja na binti yake katika ajali ya helicopter...nipigo kwetu wapenz wa mpira wa kikapu