Kobe Bryant dies in a plane crash

Kobe Bryant dies in a plane crash

1580076855248.png
 
Dah! Hii habari imenifanya nikose usingizi leo. One of the Saddest News in the history of basketball. Rest Easy Champ.
 
Dah adi States ndege kama helicopter inawezaje kuanguka? Ina maana haikuwanyiwa ukaguzi wa kutosha kabla ya kuondoka?

Rest in Piece Legend..[emoji24][emoji24][emoji24]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeishi Marekani tokea mwaka 2000. Makazi yangu yamekuwa Southern California ambayo inajumuisha San Diego na jiji kubwa la pili kuliko yote USA la Los Angeles. Tokea nikiwa secondary Tanzania nilikuwa mpenzi wa mpira wa kikapu (basketball). Kwa hio nilivyofika USA na sababu maskani yalikuwa Southern Caifornia, ni wazi kwamba ushabiki wangu ulielekea kwa Los Angeles Lakers. Enzi hizo ni Kobe Bryant ndio alikuwa anatesa sana. Team yake ya LA Lakers ilitisha sana na kushinda NBA championships mwaka wa 2000, 2001, na 2002. Kobe Bryant alishinda tena NBA World Championships mwaka wa 2009 na 2010. Kweli sikufanikiwa kwenda kuona mechi live sababu ya majukumu mengi mtu ukiwa nchi za watu. Lakini nilikuwa naangalia mechi sana muda mwingi kupitia runinga na LA Lakers wakishindwa roho ilikuwa inauma.

Leo nilivyopata habari za kifo cha champion KB anayefahamika kwa jina la Black Mamba sababu alitesa watu kama vile nyoka wa black mamba anayomwaga sumu na kukumaliza mara moja, niliumia sana sababu nimekuwa nikimfuatilia mchezaji huyo sana na alitupatia burudani ya nguvu sana mashabiki wa mpira wa kikapu.

Kobe Bryant amefariki akiwa na utajiri mkubwa zaidi ya ule wa Bakhresa au wa Mengi. Thamani yake ni US$500 million katika kifo chake. Hiyo inaonyesha mali si kitu, wote tutaelekea tu huko. Huwa jamaa hata akienda kufanya mazoezi kwa gym ya LA lakers au kwenda Staples center uwanja wa kikapu kucheza, alikuwa anasafiri na hellicopter tu. Huwa hachukuagi gari jamaa hata kama sehemu sio mbali. Kweli inasikitisha sana kwamba usafiri alioupenda sana ndio umemuua. Mtoto wake mwenye umri wa miaka 13 anayeitwa Gianna amefariki pia. Chanzo cha ajali hio kinafanyiwa utafiti.

RIP Black Mamba!

kobe-bryant-helicopter.jpg

Aina ya hellicopter iliyomuua KB24
kobe bryant.jpg

Kobe Bryant akiwa na mwanae Gianna ambaye pia amefariki leo. Watu wengine watatu wamefariki pia katika ajali hio ya hellicopter.

kb 24 second.jpg

Picha ya ajali hio
kb 24 1.jpg

Njia ya hellicopter iliyoanguka
 
mwanamichezo nyota wa mpira wa kikapu nchini marekani katika ligi maarufu ya nba amefariki pamoja na binti yake katika ajali ya helicopter...nipigo kwetu wapenz wa mpira wa kikapu
images.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msiba Mzito Sana kwa familia ya Kobe kuondokewa na Baba na Binti kwa wakati mmoja.

Ndio maana wanashauri kupanda Ndege/Helcopter kwa familia nzima ni hatari au Kusafiri kwa basi moja familia nzima ni hatari.
 
..Greatest Laker of all time.

..Kobe Bean Bryant " Black Mamba."

..MUNGU awalaze mahali pema Peponi wote waliofariki ktk ajali hii.
 
Back
Top Bottom