Habari za muda huu wadau na wafuatiliaji wa habari za ma'celebrities..I hope mko poa.
Naam..!!Bila kupoteza muda ngoja niende moja kwa moja kwenye kusudio la huu uzi,Nimekua mfuatiliaji mzuri sana wa filamu za hapa bongo especially za Vichekesho tangu enzi za kina Marehemu King Majuto,Kingwendu,Zimwi,Sharo Millionaire,Bambo,Mtanga kina Kiwewe hadi zama za kina Tini White,Kinyambe,Ringo,Gondo.
Moja kati ya Scene au nafasi ambazo hunivutia sana ni ya Ulevi,yaani namaanisha actor/actress kuigiza kama mlevi,hii ilianza kunivutia tangia enzi za Marehemu John Walker alivokua akiimba kama mlevi,pia Radio Free Africa katika kipindi chake cha Mambo mambo siku za nyuma kikiongozwa na Charles Machogo kilikua na Segment ya Busara za mlevi,kilivutia sana.
Back to the point,Katika tasnia ya Uigizaji hasa Comedy kuna Mjuba anaitwa Masele Chapombe,huyu jamaa kaanza kitambo kuigiza kama mlevi na anajua sana hadi ilifikia kipindi nikawa naona hakuna muigizaji anaeweza kuigiza kama mlevi kumzidi yeye kutokana na kuuvaa uhusika vizuri.
Ila hapa kati katokea chalii flani ivi sijui katokea fiade gani uko!?yuko yechu na anajua sana ku'act kama mlevi,Huyu jamaa anaitwa Emilian Kobelo maarufu kama Kobelo chapombe mzee wa#Inaumagaiyo!!huyu ni Comedian,Director na Editor pia wa Tamthilia ya Maneno ya Kuambiwa,Nahisi Masele anamzidi ile kuyumba tu akiwa anatembea au kasimama ila Kobelo ana vitu vingi sana kumzidi Masele katika Scene ya Mlevi.
Je kwenu wadau mnaona nani ni zaidi ya mwenzake kukaa katika scene ya Mlevi??
@NgarenaroBoy.