Huyu Nyoka Kifutu, na nyoka ambae wamakonde humwita Namalutu, ndiyo nyoka wanaongoza kwa kuwagonga watu huko Mtwara, hususani wilaya ya Newala na Tandahimba.
Ni nyoka ambao akikugonga wana tiba mzuri tu ya kienyeji, na hakuna ulemavu.
Pia kuna kinga ya nyoka, ukipewa inafanya kazi kwa muda fulani aidha, inakulinda kwa miaka mitatu, alafu inaisha nguvu, mpaka uchanjwe tena.
Ipo ambayo nyoka akikugonga, sumu haikudhuru, na ipo nyingine, unapokaribia eneo ambalo nyoka yupo, ama nyoka anapokukaribia, hukia harufu, ya kihadui hadui ambae hamuoni, hivyo anachofanya ni kuondoka eneo hilo kwa haraka.