Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Wasimuliaji wengi humu hawajawahi kumuona koboko isipokuwa wanaeleza kutokana na story wanazosimuliwa na waliosimuliwa. Ukweli ulio wazi chance ya kukutana na nyoka huyu huwa ni ndogo mno. Na kwa baadhi ya maeneo u kibahatika kumuona basi unashauriwa kwenda kwa wataalamu.
 
Mimi nishamuona,
 
Upo sahihi kabisa hasa point no. 2
 
Ukimuona unaenda kwa wataalam kufanyaje?
 
Mmoja wao alishakufa na sumu😂😂
 
Huyo nyoka ni mpole sana, mimi nimewahi kukutana naye,nafikiri labda umchokoze, ila kama hujamchokoza, Hana shida na wewe
 
I
Kweli Mwenyez Mungu kila upande kaweka maaajabu yake, tembo wanaomboleza km binadamu, tembo analia kwa uchungu

Safi sana wengi humu wanasimulia kuonyesha kwamba koboko anaonekana mara kwa kitu ambacho ni uongo. Wasimuliwaji nao wanasimulia na nina imani humu kati ya wachangiaji tuliobahatika kumuona koboko hatuwezi fika 50.Nimeishi miaka mingi maeneo yenye sifa ya kuwa na koboko ila mimi na mdogo wangu tulibahatika kumuona akimfukuza mama mmoja shambani tulipokuwa tunapanda mahindi. Yule mama alikuwa shamba jirani na sisi ghafla tukasikia sauti akiomba msaada na wakati huo yule koboko rangi ya kijivu alikuwa umbali kama mita 50 akimfuata yule mama, ponapona ya yule mama tulivyosimuliwa ni baada ya kuingia kwenye nyumba ya kigagula mmoja aliyekuwa anaishi hayo maeneo ambapo inasidika kaweka zindiko nyumba yake. Yule nyoka tulibahatika kumuona mara moja tu katika miaka 10 tuliyoishi Tabora. Ila kilichonishashangaza ni namna anavyoteleza kwenye matuta.
 
Sijaelewa ulichokiandika mkuu
 
Kuna siku nilienda kuangalia shamba Fukayosi( Bagamoyo) mida ya saa saba mchana jua kali sana.
Nilimuona black mamba mbele yangu kama hatua 30 hivi, alikua mkubwa kama futi 12. Alikua amepumzika kwenye kivuli.
Nilipomuona nilisimama sikuendelea kutembea, aliponiona akaingia kwenye shimo la kichuguu.
Humu watu wanasema black mamba anafunga kijiji sijui timbwili lake ni noma ni stori za kutunga tu.
 
We haupo sawa kichwani wenye experince ya kumuona zaidi ya mara moja wamekuja na hayo majibu, ila wewe mtafiti uchwara ndo kwanza umemuona mara yako ya kwanza unakuja na majibu yako uchwara.

na una uhakika gani kama alikua black mamba, embu ficha upumbavu wako.
 
Hadi umchokoze.... Hata mi hapo juu nimesimulia kumuona, wapo k
Lakini hadi ulianzishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…